November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jamii yatakiwa kutatua changamoto za mtoto

Na David John,Timesmajiraonile

KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16 Shirika lisilo la kiserikali la wote kwa pamoja utu(ATD) limeiomba jamii kujitathimini upya kwa kutatua changamoto zinazomkumba mtoto ili aweze kufikia ndoto zake.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Juni 13 ,2023 Mratibu Msaidizi wa Programu za kielimu ATD, Gasper Mbwambo amesema katika kusherekea siku hiyo bado mtoto yupo katika hali isiyorizisha hivyo ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anafikia ndoto zake.

Amesema katika uhalisia wa maisha bado baadhi ya watoto wako katika hali isiyoriziksha ikiwemo familia zao kuishi katika maisha duni hivyo kupelekea mtoto kushidwa kutimiza ndoto.

” Kwa pamoja tunapaswa kuungana ikiwemo Serikali, mashirika, Taasisi zisizozakiserikali kwa kuhakikisha jukumu letu ni kuhakikisha mtoto anarejeshewa haki zake”amesema

Mbwambo amesema katika kutambua hilo ATD ilianzisha mradi wa maktaba mtaa lengo likiwa kiwafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Vilevile amesema kwa ATD imejipanga kusherekea kwa kauli mbiu ya usafi na haki ya mazingira Safi na salama kwa ukuaji wa mtoto wa Dar es salaam.

Amesema kauli hiyo imelenga kuakisi mazingira ambayo yanamzumguka mtoto kila siku.

” Tumeshirikiana na Taasisi za Serikali na binafsi kwa pamoja kuhakikisha tunafikisha ujumbe katika uhifadhi wa mazingira “Mbwambo

Akiwawakilisha watoto mtoto Winefrida Noel ambaye ni mwanafunzi kutoka shule ya Hekima amesema siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ni muhimu kwa watoto ambapo aliiomba jamii na wadau wa maendeleo kuwasaidia watoto wa kike kuendelea na masomo yao.

Aidha ameipongeza Serikali kwa kuendelea kukemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii.

Naye Mhifadhi misitu kutika wakala wa Huduma za misitu Tanzania TFS) wilaya Ismail Amri amesema katika kutambua umuhimu wa maadhimisho hayo TFS imetoa miti 300 ya matunda na kivuli kwa ajili ya upandaji kama njia ya uamasishaji wa kuyapenda mazingira.

Marco Dotto Ofisa Hamasa wa Jamii kutoka Shirika la Nipefagio amesema Shirika limekuwa likiamasisha vijana mbalimbali ambapo tayari imeanza utekelezaji wa kubadilisha taka kuwa bidhaa katika mtaa wa bonyokwa na Sanawari.