December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aipa tano Yanga

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa klabu ya Yanga kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup).

KLABU ya Yanga inefanikiwa kutinga Fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 (agg-4-1) dhidi ya timu ya Marumo Gallants ambapo mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga akiwa nyumbani alipata ushindi wa mabao 2-0.

Kifuatia ushindi huo wa Yanga Sc inawafanya kuweka historia kutonga Fainali kwenye historia ya Mpira wa Miguu Tanzania.

Yanga Sc imetangulia Fainali kwa jumla ya Mabao 4-1 hivyo wataisubiri kati ya USM Alger na ASEC Mimosas ambao wanacheza baadae.