Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na wenye ulemavu, Prof Joyce Ndalichako, ametoa wito Kwa vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini kuhakikisha kuwa wanaendelea kuboresha zaidi elimu ya ujuzi Kwa vijana ambao wapo ndani ya vyuo vyako ili kuzalisha wataalam wenye ujuzi wa kushindana katika soko la ajira mwenye Nyanja za kimataifa
Pro Ndalichako ameyasema hayo Mapema Jana ijini Arusha,akifungua kongamano la elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Amedai kuwa Kwa Sasa ni muhimu wadau kuangalia namna ya kushirikiana kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ili yawe na ujuzi unaohitajika huku akisisitiza malengo ya serikali katika sekta ya elimu ni pamoja ya kuhakikisha elimu inatoa ujuzi na nguvukazi inayohitajika katika soko la ajira.
“Kila mmoja wetu ameshawai kupokea malalamiko kutoka kwa waajiri wakisema kwamba wahitimu hawana ujuzi unaotakiwa,hii ni zaidi ikiwemo kwenye sekta ya kilimo,uchukuzi,utalii,usafirishaji,muweke mikakati ya kuangalia namna ya kuimarisha ujuzi kwa vijana ambao unatakiwa katika soko la ajira ili watumie ujuzi huo katika kuleta tija na maendeleo,”amesema
Katika hatua Katibu Mtendaji wa NACTVET,Dk Adolf Rutayuga,amesema kongamano hilo limeshirikisha wadau zaidi ya 300, kutoka ndani na nje ya nchi ambao watajadiliana mada mbalimbali zinazohusu ujenzi wa ujuzi na umahiri kwa vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi.
Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa rasilimali na miradi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Masoni Nyirenda,amesema kuwa wanasimamia mfuko wa kuongeza ujuzi ambao unafadhili taasisi mbalimbali za mafunzo kwa ajili ya kusaidia vijana waweze kupata mafunzo na kujenga uwezo wa taasisi kuweza kutoa elimu yenye ubora ya ujuzi.
“Tunajua mausala ya ajira nchini yamekuwa changamoto na suala la ujuzi lilionekana ni changamoto kubwa sana kwa hiyo kupitia mfuko ule tumefadhili vijana zaidi ya 48,000 nchi nzima kupata mafunzo ya ujuzi,”amesema
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa