November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kanisa laweka jiwe maalumu kabla ya kukamilika

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

KANISA la Amani Christian Centre (TAG) lililopo Tabata jimbo la mashariki jijini Dar es salaam limeweka jiwe maalumu lenye kubeba maono kwa waumini wa dini hiyo baada ya kufanikisha hatua kubwa ya ujenzi huo linategemea kukamilika ifikapo mwaka 2025 .

Imebainika kuwa ujenzi wa kanisa hilo umetokana na nguvu ya wahisani na washirika mbalimbali ambapo imegharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi bilioni 1 na milioni mia 5.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe hilo jijini, Askofu Laurent Kameta amesema hivi sasa imefikia miaka ya ujenzi wake na limehudumu miaka13 toka kuanza kwake, lengo kuu ni kumtafuta mungu na nguvu zake.

“Jiwe hili linalowekwa ni jiwe maalumu ambalo huwakilisha wajibu wa mungu ambapo moyo wa mwanadamu upo katika kumtumikia mungu, ” amesema Askofu Kameta

Aidha Kameta ameeleza kuwa Kanisa likitumika vizuri linakuwa kama shule na kichocheo ama kiini kikubwa cha mabadiliko kwa waumini wake ambapo kanisa hilo lina mitambo ya sauti, CCTV camera , runinga na tahadhari za moto.

Hata hivyo askofu huyo amewashukuru kwa namna moja ama nyingine kampuni ya Nangai construction iliyohusika katika kusimamia na kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo.

Kwa upande wa Serikali mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ilala Adrian Kishe amewapongeza waumini wa Karisa hilo kwa jitihada mbalimbali za kufanikisha harambee dhidi ya ujenzi huo.

Nae mwakilishi kutoka kamati ya Amani ambaye ni mratibu wa chavifmat, Sheikh Yahya Hussein mbali na kulipongeza kanisa alihimiza juhudi na jitihada katika kuwainua vijana kupitia sekta mbalimbali hususani ajira.

Mbali na uwekaji wa jiwe la msingi dhima kubwa ilikuwa kuangalia tulikotoka, tulipo sasa na tunako elekea hafla hiyo ilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo upande wa Serikali, maaskofu,Mapadri,Mashekh na waumini kutoka dini na madhehebu tofauti.