November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazee, Wajane watakiwa kudumisha Umoja, Mshikamano

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

DIWANI wa kata ya Ilala ,Mjumbe wa Baraza Kuu la CCM Taifa Saady Kimji, amewasaa Wazee na Wajane wa Kata ya Ilala kudumisha Umoja na Mshikamano katika kuisaidia Serikali ya chama cha Mapinduzi Utekelezaji wa Ilani .

Diwani Saady Kimji, alisema hayo Kata ya Ilala wakati wa kutoa sadaka ya Futari kwa kushirikiana na wadau wa MAENDELEO Fedha Intenational School kwa Wazee wa Ilala na Baadhi ya Watu wenye Uhitaji Maalum .

“Wazee Wangu wa Ilala na ndugu zangu wenye mahitaji Maalum leo nimewaita tumejumuika pamoja kupeana sadaka ya Futari ambayo tumeshirikiana na Wadau Wetu Shule ya Fedha Itenational nawaomba Wazee Wangu wa Ilala mpokee hichi kidogo nawaomba mdumishe Umoja na Mshikamano tujenge Ilala Yetu ” alisema Kimji .

Diwani Saady Kimji alielezea Maendeleo ya Kata ya Ilala vipaumbele walivyojiwekea sasa katika Utekelezaji wa Ilani kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , ameshapeleka fedha kwa ajili ya Zahanati ya ilala ambayo inajengwa eneo la Bungoni itarahisisha kutatua kero wananchi wa Ilala ambao walikuwa hawana Zahanati wala kituo cha afya.

Alisema Zahanati hiyo ambayo inajengwa itakamilika mwaka huu iweze kutoa huduma za Mama na Mtoto

Aidha alisema mtaa .
Sharifu Shamba Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa inajengwa karibu itakamilika iweze kutoa huduma .

“Mtaa wa Mafuriko barabara imejengwa kwa kasi ni kazi ya Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu fedha za Tozo shilingi milioni 500 ambazo zimetolewa na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, kila Jimbo na barabara imeshapewa jina la Kasongo “alisema.

Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji(Katikati) akikabidhi futari kwa Wazee wa Kata ya Ilala katika mfungo huu wa mwezi wa Ramadhani futari hiyo imetolewa kwa Ushirikiano wa shule ya Fedha International.
Diwani wa Kata ya Ilala Saady kimji (Katikati) akiwa na Viongozi wa Kata ya Ilala Wakati wa Kugawa futari kwa wazee iliyotolewa kwa Ushirikiano wa shule ya Fedha Internationl