Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti wa Umoja wanawake (UWT) Wilaya ya Ilala Neema Kiusa , amewataka Watanzania kuishi katika matendo mema ambayo yanampendezesha Mwenyezi Mungu kuacha kuishi kwa kufuata utamaduni wa kuiga badala yake tuishi kwa kufuata Mira za kitanzania.
Mwenyekiti wa Umoja WANAWAKE WIlaya ya Ilala Neema Kiusa, alisema hayo Jimbo la Ukonga kituo cha Afya nguvu Kazi Chanika katika madhumisho ya Siku ya matendo mema Dunia ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo ambapo walishiriki Shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti na shughuli za Usafi .
“Dunia kwa sasa imeharibika viongozi wa dini na Walezi tuwe karibu na watoto wetu tuishi katika misingi Bora ya kumpendezesha Mwenyezi Mungu ikiwemo kufuata mira na Desturi za Kitanzania” alisema Neema .
Mwenyekiti Neema aliwataka wazazi na Walezi wawalehe watoto wao katika misingi Bora Ili watoto wetu waweze kujitambua na kuwataka watoto walindwe wasinyanyaswe Ili kupata Taifa Bora .
Akizungumzia Kampeni ya upandaji miti ambavyo amezindua Jimbo la ukonga iliyoandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo alisema amepongeza Taasisi hiyo kwa kuunga mkono Juhudi za serikali katika sekta ya utunzaji mazingira Fahari Tuamke Maendeleo imekuwa mstari wa mbele.
“Suala la kupanda miti ni jukumu letu sote tuishi katika Mazingira Bora ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kila mkoa na WIlaya zipande miti Kila mwaka Ili kulinda Mazingira na vyanzo vya maji ” alisema.
Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alisema leo ni Siku ya matendo Mema Duniani wameungana na Umoja WANAWAKE WIlaya ya Ilala UWT katika Shughuli za kijamii usafi Usafi pamoja na kupanda miti ya matunda na kivuli .
Neema Mchau alisema ukitenda mema matendo ya ukatili kwa Jamii yatapungua ambapo alitoa wito kwa serikali na Jamii kutenda mema kuondokana na matendo ya ukatili .
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Chanika William Mwilla alisema Wananchi wa Chanika wameungana na Taasisi ya Fahari kwa ajili ya MAADHIMISHO ya Siku ya matendo mema Duniani kwa kuzindua Kampeni ya kupanda miti Jimbo la Ukonga na kufanya usafi kituo cha Afya .
Mwenyekiti Mwilla alisema CCM Chanika ipo na serikali Pamoja katika kusimamia utekelezaji wa Ilani na kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria