Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
TUZO ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu yenye lengo la kukuza Sekta ya uandishi, uchapishaji au usambazaji wa vitabu nchini kuweka rekodi mpya April 13, 2023 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Msumbiji Mheshimiwa Joaquim Chissano.
Aidha, Tuzo hiyo inalenga kukuza ari ya usomaji nchini itatolewa kwa mara ya kwanza tokea kuzinduliwa kwake Septemba 12, 2022 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Hivyo, tuzo hiyo imepewa jina la Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kumuenzi Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mwandishi wa mashairi na mfasiri wa tamthiliya, pia Mwl. alikuwa kiongozi aliyekuza mawazo huru na kuchochea kwa kiwango kikubwa kukua kwa lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa na Kimataifa.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano