Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta miradi mikubwa ya Maendeleo Kata ya Ilala Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam.
Diwani Kimji ,alitoa pongezi hizo Wilayani Ilala alipofanya ziara ya kikazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo .
“Wananchi wa Kata ya Ilala tunampomgeza Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hasaan, pamoja na Mbunge wetu wa jimbo la Ilala Mussa Zungu, kwa kuleta maendeleo mikubwa Kata hii ya ya Ilala ” alisema Kimji.
Diwani Kimji alisema katika kata ya Ilala Serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mbali mbali ya Maendeleo ikiwemo Barabara ya lami,Ofisi ya Serikali ya Mtaa ya Sharifu shamba na ujenzi wa Zahanati ya kisasa kata ya Ilala
Akielezea changamoto za kata ya Ilala alisema ajira kwa Vijana ,utililikaji maji taka kwa baadhi ya mitaa ,uchakavu wa Barabara ambazo zimechoka pia azipitiki kama sadan Songea .
Akizungumzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt ,Samia Suluhu Hassan alisema anafanya kazi kubwa katika Utekelezaji wa ILANI ya chama na kuleta Maendeleo katika Miradi mikubwa Ikiwemo ya Sekta ya elimu ,Afya na Barabara Miundombinu na madaraja ya kisasa katika nchi yetu .
Pia alisema Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kukuza Uchumi na kuleta fursa mbalimbali Ikiwemo Sekta ya Utalii amewataka Watanzania tumuunge MKONO na kisimamia Miradi ya Maendeleo ambayo imetekeleza Kila kata .
Akizungumza na Diwani wa Ilala Mkuu wa WIlaya Ilala Edward Mpogolo alisema atampa Ushirikiano wa kutosha na kumueleza kuwa anatarajia kufanya Ziara za Maendeleo kata ya Ilala Ikiwemo za kutatua kero za wananchi .
More Stories
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo