November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mfumo wa Mshitiri kuondoa changamoto ya dawa

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa

WATENDAJI na wataalamu wa afya mkoani Rukwa wametakiwa kuutumia vyema mfumo mpya wa Mshitiri katika kuagiza dawa ili kuondoa changamoto ya madeni inayojitokeza kwa Wazabuni wakati wa kuagiza dawa kupitia mfumo uliopo.

Wito huo umetolewa na katibu tawala msaidizi mkoa Rukwa Samson Hango wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa mfumo wa mshitiri  kwa watendaji na wataalamu wa afya mkoani Rukwa ambapo amesema kuwa mfumo huo utakwenda kutatua tatizo kubwa la madeni linalojitokeza kila wakati kwa wazabuni wa dawa nchini.

Alisema kuwa kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa Wanananchi  kuhusu kukosekana kwa dawa na vifaa tiba kwenye baadhi ya vituo vya afya ,zahanati na hosipitali nah ii yote inatokana na usimamizi mbovu wa makusanyo na na uagizaji wa dawa na kuwa jibu la tatizo hilo ni matumizi ya mfumo wa mshitiri.

Hango ambaye pia ni ofisa elimu mkoa Rukwa alidai kuwa wao kama wawezeshaji ngazi ya mkoa wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wahusika katika eneo hilo la usimamizi wa mapato na uagizaji dawa wanapata elimu ya kutosha  juu ya mfumo huo mpya wa uagizaji dawa na kuwa sasa hakuna njia nyingine itayotumika katika zoezi hilo kinyume na mfumo huo wa Mshitiri.Hivyo pia aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kusimamia kikamilifu afua mbalimbali za mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya ikiwemo kufanya ukaguzi wa kitabibu.

katibu tawala msaidizi wa mkoa Rukwa Samsong Hango akifungua mafunzo kwa Watendaji na wataalamu wa afya juu ya mfumo wa mshitiri