Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
WAZAZI na walezi wa watoto walioko shuleni wametakiwa kuwaongoza vizuri watoto wao na sio kutowakatisha tamaa ili waweze kutimiza ndoto zao kimaisha punde wamalizapo shule.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mohamed Nassoro Hamdan (Meddy) alipokuwa akizungumza katika mahafali ya pili ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Idete iliyoko Wilayani Uyui, Mkoani Tabora.
Alisema serikali ya awamu ya sita imesikia kilio cha wananchi na kuamua kuondoa ada zote kuanzia shule ya awali hadi kidato cha 6 ili watoto wote wapate elimu, hivyo jukumu pekee la wazazi ni kupeleka watoto wao shule na kuwahamasisha kusoma kwa bidii.
Alibainisha kuwa elimu ni urithi mzuri kwa mtoto, hivyo kama wataongozwa vizuri katika makuzi yao na kupata elimu watapata mwanga mzuri wa maisha utakaowawezesha kutimiza ndoto zao watakapokuwa wakubwa.
‘Elimu ndio urithi mzuri wa kumwachia mtoto, tusiwakatishe tamaa bali tuwaongoze vizuri kwa kuwapeleka shueni na kuwahamasisha kusoma kwa bidii, hakuna kisingizio cha ada tena, serikali imewarahisishia kila kitu’, alisema.
Ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo wanafanya vizuri katika masomo yao, Meddy alisema wanapaswa kula vizuri na kulala mahali pazuri, hivyo akaendesha harambee maalumu iliyowezesha kupatikana fedha za kununulia vitanda 46
Awali akimakaribisha mgeni rasmi (MNEC), Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Paul Mdaki alisema wamewaandaa vizuri watoto wao na ana uhakika wote watafanya vizuri na kuendelea na masomo katika Vyuo mbalimbali ikiwemo Vyuo Vikuu.
Alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 162 wanahitimu kidato cha sita mwaka huu katika shule hiyo na kama ilivyokuwa mwaka jana wote wamewapika vizuri na watafaulu na kuendelea ngazi za juu.
Aliongeza kuwa shule hiyo ina maendeleo mazuri sana kitaaluma kwani mwaka jana ilishika nafasi ya 1 ki-wilaya, ya 7 Kimkoa na ya 144 Kitaifa kati ya shule 644 na mwaka huu ana uhakika watapanda zaidi.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â