Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza
Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia,Jimbo la Ilemela limepokea fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ambapo zaidi ya bilioni 4.6 zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ardhi kwa ajili ya kupanga na kupima viwanja kwa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.Lengo la zoezi hilo kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia ardhi yao huku ikitoa fedha nyingine katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu kwa Wilaya hiyo.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyasaka alipofanya ziara kwenye Kata ambapo alifanya kupitia mkutano uliofanyika uwanja wa Mkombozi.
Dkt.Angeline ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia ametenda mambo makubwa katika Jimbo la Ilemela kwa kuwapatia fedha nyingi za maendeleo katika sekta mbalimbali.
Ambapo ameeleza kuwa kwa kipindi hicho jimbo hilo mbali na kupatiwa fedha katika sekta ya ardhi pia katika sekta ya afya wamepatiwa kiasi cha bilioni 2.25 huku sekta ya elimu msingi kiasi cha zaidi ya bilioni 1 na elimu sekondari bilioni 1.250.
Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kukemea vitendo vya unyanyasaji na ukatili vinavyoendelea katika jamii huku akisisitiza wananchi kuripoti polisi kila vinapojitokeza vitendo hivyo.
Pamoja na kuwahimiza vijana kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na halmashauri kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyasaka Abdulrahman Simba,ameeleza kuwa ndani ya Kata hiyo serikali imewapatia kiasi cha zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo hivyo ameishukuru serikali pamoja na Mbunge huyo kwa jitihada za kuwaletea wananchi maendeleo.
Awali Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava amempongeza Mbunge huyo kwa juhudi zake katika kuwahudumia wananchi na kutatua kero zao na Serikali ya wilaya iko pamoja nae.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Afisa Maendeleo wa Manispaa hiyo Sitta Singibala amewaasa wananchi kutumia mikutano ya hadhara kwaajili ya kunufaika na mfuko wa maendeleo ya jamii wa kuhudumia kaya masikini TASAF kwa wale wenye sifa.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula katikati wakati alipofanya ziara yake Kata ya Nyasaka na kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Mkombozi.
Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Ilemela Godfrey Mzava, akizungumza wakati Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula alipofanya ziara yake na kuongea na wananchi wa Kata ya Nyasaka.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria