November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Simbu, Clara Luvanga wanamichezo bora Tanzania 2022

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Mwanariadha Alphonse Felix Simbu, ameshinda Tuzo mbili za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mwanariadha Bora wa Kiume na Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2022.

Katika sherehe hizo zilizofanyika usiku wa jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mshambuliaji wa Yanga Princess, Clara Luvanga ameshinda tuzo mbili pia, Mwanamichezo Bora wa Kike na Mwanasoka Bora wa Kike.

Tuzo nyingine ni Aishi Manula (Mwanasoka Bora Mwanaume 2022), Failuna Abdi (Mwanariadha Bora wa Kike 2022), Ibrah Class (Bondia Bora Ngumi za Kulipwa 2022), Rehema Suleiman Said (Mchezaji Bora wa Tenisi kwa Walemavu) na Sophia Latiff (Muogeleaji Bora).

Aidha, timu za Taifa za Kuogelea na Soka ya Walemavu ‘Tembo Warriors’ pamoja na klabu ya Simba Queens nazo zilikabidhiwa tuzo kwa kuiwakilisha nchi vizuri mwaka jana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alikabidhiwa Tuzo kwa mchango wake mkubwa kwenye Michezo, Sanaa na Uatamduni nchini.

Tuzo yake ilipokewa na na mgeni rasmi, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Pindi Chana aliyeongozana na Naibu Waziri wake, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga.