Na mwandishi wetu, Timesmajira Online
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zimeongeza ari kubwa kwa wachezaji kuipigania timu yao.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe, wakati wa uchezeshaji wa droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya robo fainali, iliyofanyika jana katika ofisi za Azam Media.
Salehe alisema kipindi cha nyuma timu yao ilikuwa inaishia hatua ya awali ya michuano ya Kimataifa, lakini sasa vijana wamekuwa na hamasa kubwa ya kuipigania nembo ya timu yao.
“Sisi kwa sasa tunashukuru kwa hamasa hii, unawaona kabisa wachezaji wanavyopambana ili kuipatia timu matokeo mazuri uwanjani, hivyo tunashukuru kwa kila kitu kinachochangia ushindi wetu.
“Historia imebadilika na wakati huu tunaenda kwenye mechi ya mwisho wa wiki tukiwa na shauku kubwa ya kuona timu yetu inashinda mbele ya wageni wetu US Monastir, mchezo utakaopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam,” Amesema.
Yanga na Simba wanaogelea bahari ya fedha za Rais Samia aliyeahidi kununua kwa Sh Milioni 5, kila goli linalopatikana kwa timu hizo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship