NA
MWANDISHI WETU, LUSHOTO
WAJUMBE
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wametembelea
kiwanda cha kuchakata Chai Mponde kilichoko Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Machi
16, 2023 ili kukagua utekelezaji wa miradi mitano inayotekelezwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) na taasisi zilizo
chini yake.
Kiwanda
cha Chai Mponde kinamilikiwa kwa ubia na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) taassi ambazo
ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
(OWK-KVAU), kila taasisi inamiliki asilimia 42% ya hisa na Msajili wa Hazina(TR) asilimia 16%.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa
Joyce Ndalichako, Naibu wake Mhe. Patrobas Katambi, Katibu Mkuu Profesa Jamal Katundu na Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi
hizo, CPA. Hosea Kashimba (PSSSF) na Dkt. John Mduma (WCF) pia walikuwepo
wakati wa ziara hiyo.
Kiwanda
cha Chai Mponde kilifanyiwa ukarabati mkubwa baada ya kusimama kufanya kazi kwa
kwa zaidi ya miaka 10, tayari kimeanza kazi ambapo kilo 24,460 zimeuzwa na tani 50
zinategemewa kuuzwa mwishoni mwa mwezi Machi, 2023.
Aidha
Wajumbe wa Kamati wameipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kuruhusu uwekezaji kwenye
kiwanda hicho kwani kitanufaisha wakulima wa Chai wa Halmashauri ya Bumbuli na
maeneo yanayozunguka wilaya nzima ya Lushoto.
“Kwa
niaba ya Wajumbe wa Kamati nichukue fursa hii kuipongeza Serikali kwa kukubali
uwekezaji huu, kwani unakwenda kuleta manufaa makubwa kwa wakulima wa chai.”Alisema
Mhe. Fatma Tawfiq, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na
Maendeleo ya Jamii.
Aidha Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Riziki Lulida licha ya kupongeza alishauri uongozi wa kiwanda kutoa ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu.
Akiongea
kwa niaba ya wawekezaji Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), Dkt. John Mduma alisema, kusudio kubwa la kukifufua kiwanda ni
kuwawezesha wananchi wa Lushoto, Bumbuli Korogwe na maeneo jirani kupata kipato
na hivyo kuwainua kiuchumi kwani wengi wanategemea zao hilo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi