Judith Ferdinand na Daud Magesa,TimesMajira Online,Mwanza
WAZIRI Mkuu,Kassim Majaliwa,amewataka watanzania kutafakari kwa kuzingatia sheria na matumizi sahihi ya barabara ili kubabiliana na ajali za barabarani.
Ameeleza jukumu la usalama wa barabarani ni la kila mmoja hivyo washirikiane katika kuelimisha na kuonyana,kwani takwimu za ajali barabarani kwa miaka mitatu 2020 hadi Desemba 2022 zimeongezeka na kusababisha vifo vya watu wengi huku wengine wakibaki na ulemavu wa kudumu.
Majaliwa ameeleza hayo wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, ambayo yalianza Machi 13 hadi 17 mwaka huu,katika uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela, yakiwa na kauli mbiu ikiwa “Tanzania bila ajali inawezekana,timiza wajibu wako.”
Majaliwa ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu jumla ya ajali 5132 zilizofikishwa kwenye vyombo vya usalama na kutolewa taarifa huku ajali hizo zimegarimu maisha ya watu jumla 4060, na kusababisha majeruhiwi na walemavu 6427.
“Ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo cha maumivu na majonzi kwa jamii,kupoteza wa wapendwa wetu,mali,vyombo vya moto na ulemavu wa kudumu kwa ndugu zetu,zinaua na kupoteza nguvu kazi nyingi ikiwemo wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wakti mwingine ata wanafunzi wa taaluma ya makundi mbalimbali,”ameeleza Majaliwa.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Jeshi la Polisi nchini kuhusu ajali za barabarani kwa takribani miaka mitatu iliopita,ajali zimeongezeka kwenye maeneo mbalimbali hasa eneo la abiria.
“Eneo hili la abiria 1,582 wamepoteza maisha idadi hii ni kubwa sana katika hili lazima tuunganishe nguvu zetu,abiria 1,372 walipata majeraha mbalimbali kwenye miili yao ikiwemo ulemavu,”ameeleza Majaliwa na kuongeza
“Tunao wajibu wa kuhakikisha idadi hii ya vifo na majeruhi inapungua,kwa kufua sheria na kanuni za matumizi ya barabara sahihi,” ameeleza Majaliwa.
Kwa upande wa watembea kwa miguu Majaliwa ameeleza kuwa kwa kipindi hicho cha miaka mitatu watembea kwa miguu 959 walipitiwa na vyombo vya usafiri walipokuwa wanatembea barabarani huku 650 walijeruhiwa kutokana na ajali za barabarani wakitembea kwa miguu.
“Idadi hii nayo haipendezi kuitamka ni kubwa tunapotumia vyombo vya moto barabarani lazima tuhakikishe tunazingatia watembea kwa miguu,na wale wanaotembea kwa miguu kando kando ya barabara lazima wazingatie matumizi sahihi ya barabara,”ameeleza Waziri Mkuu.
Pia ajali za waendesha pikipiki kundi hilo siyo tu waendesha bodaboda hao kwa ajili ya biashara hata wale wanaofanya kwa matumizi binafsi kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu wapanda pikipiki 797 walifariki huku 725,walijeruhiwa.
Kundi jingine ni wapanda baiskeli ambao kwa kipindi hicho 196 walipoteza maisha na wengine 82,walijeruhiwa idadi hiyo nayo siyo nzuri pia.
Aidha Majaliwa ameeleza kuwa kwa upande wa wanaoendesha vyombo vya moto katika kipindi hicho madereva 509 wamepoteza maisha huku 584 wakipata majeruhi mbalimbali katika miili yao wakiwa wanaendesha magari huku kundi jingine ni la wavuta na watembeza mikokoteni 17 walipoteza maisha na 14 walipata madhara miilini mwao.
“Nimeonesha idadi hii kwa makundi ili na nyie mpate picha ya namna ajali zinavyojitokeza kwenye maeneo mbalimbali,hakika tunahitaji jitihada za pamoja za kuhakikisha tunakabiliana na ajali hizi katika kipindi cha miaka mitatu pekee jumla ya ajali zote 5132,ambazo zilimudu kufikishwa kwenye vyombo vya usalama na kutolewa taarifa, zimegarimu maisha ya watu jumla 4060, na kusababisha majeruhi na walemavu 6427,”.
Sanjari na hayo Waziri Mkuu ameliagiza jeshi la polisi na wasimamizi wengine wa sheria kuhakikisha kampuni za mabasi yanayofanya safari za mwendo mrefu kuwa na madereza zaidi ya mmoja ili kuepuka ajali hizo.
“Uchunguzi unaonesha kuwa mabasi yanaoenda safari ndefu ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajali za barabarani hivyo utaratibu uliotolewa na jeshi la polisi kuwa katika basi kuwe na dereva zaidi ya mmoja,makampuni na wamiliki wahakikishe wanaajiri madereva zaidi ya mmoja ambao wa safari ndefu kwa ajili ya usalama wa abiria kwani kuwa na dereva mmoja ni uzembe na haikubaliki,”
.Serikali itaendelea kuboresha miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji lengo ni kukuza shughuli za usafirishaji kuwa nzuri na magari kupita katika barabara nzuri.
“Tunaendelea kuweka alama za barabari ambazo ni muhimu kwa wananchi kuzijua hivyo tumieni fursa hii ya maadhimisho kujifunza kwa kupita katika banda la TANROADS na Polisi ili mfahamu mnapokutana nazo huko barabarani zina maanisha nini,”.
Pia Majaliwa katumia fursa hiyo kuitaka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,kuingiza elimu ya usalama wa barabarani na matumizi sahihi ya barabara kwenye mtaala wa elimu ili elimu hiyo ianze kufundisha katika shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo ili watoto wajifunze na kuwa na uelewa tangu wakiwa wadogo na kusaidia kuepesha taifa na ajali za barabarani zinazoua nguvu kazi ya taifa.
Vilevile wananchi wanapotumia barabara kuzijua sheria na kanuni za usalama wa barabarani,kutoshabikia mwendo kasi,kuhakikisha wanatumia barabara kwa kutumia vivuko vya watembea kwa miguu ambavyo vina alama,kuacha kuendesha baiskeli na mkokoteni katikati ya barabara kuu pamoja na kutotelekeza magari mabovu barabarani bila kuweka alama na kuepuka kuwaacha Watoto wadogo bila kuwa na wasimamizi.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapindu(CCM),Mkoa wa Mwanza Reuben Sixbert Bado tunachangamoto sana sisi watumiaji wa barabara ili kupunguza ajali zinazokuwa zinatokea elimu iliyotolewa katika maadhimisho hayo ingesambaza kwa watu wote ikiwemo wenye vyombo vya moto.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria