Na David John, Timesmajira Online
MKUU wa Wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya Kanali Denis Mwila amewataka wananchi kushiriki katika ulinzi wa vyanzo vya Maji hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere ambalo kukamilika kwake linategemea kizalisha umeme MEGAWATI 2115.
Amesema kuwa kukamilika Kwa Bwawa la Julius Nyerere Kwa kiasi kikubwa kutachangia kukua Kwa uchumi lakini pia kuwezesha kupatikana umeme wanuhakika katika nchi hivyo lazima vyanzo vya Maji vilindwe na yeyote atakae haribu miundombinu hatua kali za kisheria lazima zichukuliwe.
Kanali .Mwila ameyasema haya Leo Machi 8 ofisini kwake mara baada ya kutembelewa makundi ya watalamu mbalimbali ikiwemo watalaamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Baraza la Mazingira NEMC, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA ,waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali nchini,pamoja na watalaamu wan Bodi ya Maji Bonde la Rufiji mkoani Iringa.
“Bwawa hili lilikuwa kwenye Mpango wa kujengwa Kwa miaka mingi na leo kiazia Serikali ya awamu ya Tano na hivi awamu ya sita mradi unatekelezwa hivyo niwajibu wa Kila mtanzania kuhakikisha analinda vyanzo vya Maji ili kuwezesha Bwawa la Julius Nyerere kukamilika Kwa wakati.”amesema Kanali Mwila
Nakuongeza kuwa ” inasikitisha kuona kuna watu wachache wanaingia kwenye vyanzo vya Maji na kuleta uharibifu mkubwa ambao unaweza kuhatarisha utekelezaji wa mradi mkubwa ambao ndio miongono mwa kipaumbele kwenye taifa .
Akizungumzia wananchi ambao wanachepusha Maji Kwa ajili ya shughuli za Kilimo kupitia Bonde la Usangu katika mto mbarali kuacha mara moja na wao kama Wilaya wataendelea na uperesheni ya kuhakikisha watu hawaharibi vyanzo vya Maji kwenye mto mbarali ambao Maji yake yanakwenda kujazwa katika mto rufiji
Pia kuhusu migogoro ya mara Kwa mara Wilaya humo hususani kwenye eneo la Ardhi Kanali amesema Serikali inachukua hatua na kimsingi changamoto hizo zinaelekea kwisha japo kuwa mchakato wake ni mkubwa.
“Mnajua mbarali Kuna Bonde la Usangu ambalo watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu wanafika kuja kufanya shughuli zao hususani kilimo hapa na kimsingi hakuna Serikali ambayo ipo Kwa ajili ya kukandamiza wananchi wake na kusigana hakuleti tija katika nchi.”amesema
Wakati huohuo Kanali Mwila ametoa ushauri Kwa wananchi na waandishi wa Habari nchini kuwa wazalendo na kutanguliza maslahi ya taifa mbele na hasa kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwamo Bwawa la Julius Nyerere ambalo kukamilika kwake kutaleta neema kubwa kwenye nchi.
Amesema Yako mambo muhimu ambayo yanatakiwa kuzungumzia kizalendo ikiwamo mambo ambayo ni kipaumbele Kwa nchi ikiwamo Bwawa la Julius Nyerere ambapo kwasasa Serikali dicho lake lipo kwenye utekelezwaji wa mradi huo mkubwa.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya Mbarali Missana Kwangura.amesema kuwa wataendelea kushirikiana na watalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji ili kuhakikisha Kila kitu kina kuwa sawa na ikiwamo pia upandaji wa miti ambayo ulinzi mkubwa wa utunzaji wa vyanzo vya Maji kwenye mto mbarali.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi