Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
BARAZA la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC)limesema jitihada za serikali za kusisitiza usafi wa mazingira zimeleta mafanikio makubwa ikiwemo kutomeza ugonjwa wa kipindupindu ambao haujaripotiwa tena kwa miaka saba sasa.
Hayo yamesemwa jijini leo,Machi 3,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Samweli Gwamaka wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa baraza hilo katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuhamasisha usafi wa kila jumamosi na elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo jitihada hizo zimesaidia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.
“Miaka ya nyuma ikifika kipindi cha mvua lazima wapatikane wagonjwa wa kipindupindu lakini sasa hivi kutokana na elimu inayotolewa jamii imegundua kuwa ikiwa katika mazingira machafu na magonjwa yanaweza kuiandama,”amesema Dkt.Gwamaka.
Hata hivyo Dkt.Gwamaka ameeleza kuwa NEMC imepanga kuanzisha klabu za utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kuwajengea watoto msingi mzuri wa namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira katika maeneo yao.
Ameeleza NEMC inaanzisha klabu za mazingira na kuzilea kwasababu watoto wakianza kufundishwa wakiwa katika umri mdogo ni rahisi zaidi kuelewa umuhimu wakutunza mazingira na faida zake kijamii,kiuchumi na kiafya.
“Tunaenda kuelimisha na kukikamata kizazi cha watoto wadogo kuanzisha shule za msingi na sekondari ili wachukulie suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu lao la kila siku katika mwenendo mzima wa maisha yao.Tunaamini watakapo kuwa wakubwa tabia itakuwa imejengeka ,”alisema .
Dk.Gwamaka alieleza kuwa NEMC imeendelea kupokea na kushughulikia malalamiko taklibani 369 ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira kutoka kwa wananchi ikiwemo kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye bomba,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango,uchafuzi wa vyanzo vya maji,utiririshaji wa maji taka na uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwanda.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi