Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
TIMU za Friends of Tulia Trust (Wanawake na Wanaume) zimeondolewa kwenye mashindano ya Sodo 4 Climate ya Betika yenye lengo mahsusi kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira yanaendelea katika viwanja hivyo.
Mashindano hayo
yanayoendelea katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam yameenda sambamba na Kaulimbiu isemayo ‘Shabiki Soka, Sio uharibifu wa Mazingira’, ambapo yanachezwa kwa mfumo wa mtoano (Knock Out).
Hayo ameyasema Afisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar es Salaam
“Mashindano haya yanahamasisha kutunza mazingira na tayari tumetoa vifaa, elimu ili kutunza Bahari sanjari na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yamekuwa ni tatizo kubwa duniani kote,” amesema Rugambwa.
Amesema katika mashindano hayo timu ya Friends of Tulia Trust imetupwa nje ya mashindano na timu ya Espanyol kwa mabao 2-0 kwa upande wa wanaume na timu ya Wanawake kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Espanyol.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025