Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wito umetolewa wananchi hasa wale ambao Wana Meno yenye rangi nyekundu hususani kwa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanawatumia zaidi wataalamu katika kusafisha Meno Yao na kuachana na Tabia ya kusafisha Meno kiolela Kwa Sasa wapo baadhi ya watu ambao wanatumia madawa yenye kemikali Kali kwa ajili ya kungarisha Meno hayo Jambo ambali ni hatari kwa afya ya kinywa.
Hayo yameelezwa na Dkt ClaraJuliana Steven wakati akiongea na wananchi ambao waliojitokeza kwenye viwanja vya makumbusho kwenye kambii maalumu ya madaktari bingwa iliyoabdaliwa Chini ya mganga mkuu wa Jiji la Arusha.
Dkt huyo alieleza kuwa zipo sababu ambazo zinazosababisha Meno kuwa na rangi nyekundu ambapo mojawapo ni maji kuwa na Fluoride kubwa.
Alidai kwa Sasa zipo teknolojia tena za kisasa kabisa za kusafisha na kungarisha Meno hayo yenye rangi nyekundu na kuwa meupe ingawaje Napo huko mitaani kuna wanaosafisha Meno kiolela olela.
Alidai kusafisha Meno kiolela Lela kuna madhara makubwa Sana hasa kwenye afya ya kinywa na mojawapo ya madhara ni pamoja na kupasuka kwa Meno yote,kupata Magonjwa ya Kudumu ya Meno,kupata vidonda vya midomoni vya Kila mara.
Aliwahimiza wananchi kuhakikisha kabla ya kutaks kufanya huduma ya kusafisha na kungarisha Meno waweze Kwanza kuwasiliana na madaktari ambao wao ni taaluma Yao na wataweza kuwapa ushauri kabla.
Naye mganga mkuu wa Jiji la Arusha Dkt Maduhu Nindwa alisema kuwa wao kama wataalamu wa afya Wana mikakati mbalimbali ya kuendelea kutoa elimu dhidi ya kinywa kwa kuwa matatizo ni mengi Sana kwa jamii Dkt Nindwa alisema kuwa miongoni mwa matatizo hayo ya kinywa yameeeza kiwaathiri hata watoto kutokana na wazazi wao kuweza kuwapa dawa kwa kuhisia bila kumuona daktari.
“Tumeona hata hapa mojawapo ya wagonjwa ambao wanajitikeza kwa wingi Sana hasa kwenye afya ya kinywa ni watoto na tayari wameshaathurika kutoka na matumizi Mabaya ya dawa na ukosefu wa elimu niwaombe wazazi na walezi kuhakikisha kuwa kabla ya kumpa huduma yoyote ile ya Kitabibu mtoto embu Kwanza pita kwa daktari”aliongeza Dkt Nindwa.
Alihitimisha kwa kusema kuwa wao kama Jiji la Arusha wana mikakati mingi Sana ya kuendelea kuweka kambi mbalimbali za madaktari wa Magonjwa mbalimbali ambapo kambi hizo zitaweza kuwarahisishia wagonjwa kuweza kupata huduma kwa harakw ikiwa ni pamoja na ushauri kulingana na Aina ya ugonjwa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa