Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
JESHI la polisi Kikosi cha Wanamaji Dar es salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Mifugo mnamo 12/01/2023 majira ya asubuhi huko maeneo ya soko la Samaki Ferry wakiwa katika operesheni ya pamoja ya kuzuia uvuvi haramu na makosa mengine ya kijinai walifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili (2) wakiwa na samaki KG 980 zilizokuwa ndani ya boti yenye usajili nambari . Z. 103585 jina MV MAEDRA.
Samaki hao wanasadikika kuvuliwa kwa kutumia Baruti. Taratibu za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani zinaendelea. Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru na kutoa pongezi kwa wananchi wote ambao wanachukia uhalifu na linawaomba waendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahalifu hao.
Pia Jeshi la Polisi linaendelea kutoa onyo kwamba halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejihusisha na uvuvi haramu pamoja na makosa mengine ya kijinai.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini