August 16, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zimebaki siku sita uzinduzi wa JNHPP

Na.Mwandishi wetu,Timesmajira

Zimebaki siku sita tu kuelekea uzinduzi wa kihistoria wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme, hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika nchini Tanzania.

Uzinduzi huo unaashiria hatua kubwa katika safari ya Tanzania ya kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye, sambamba na kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mradi wa JNHPP ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya nishati, ukiwa na matarajio ya kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Kwa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme, mradi huo unatarajiwa kutoa nafasi zaidi kwa sekta za viwanda, biashara, huduma na uwekezaji kukua, huku ukisaidia kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na upungufu wa nishati.