November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

IJA chabaini mahitaji kwa wanaoendesha mashauri ya watoto

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

CHUO cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kimefanya utafiti na kubaini kuwa wadau wanaoendesha mashauri ya watoto wanahitaji kupata fursa za mafunzo endelevu ili kwenda na wakati katika kufanya maamuzi katika mashauri hayo.

Akizungumza leo Januari 22,2023 jijini Dodoma katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ,Mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho Roggers Ndyanabo amesema,baada ya utafiti huo wao kama chuo walitoa fursa ya kozi endelevu kwa wanaohusika katika mashauri hayo.

Aidha amesema,pia wamefanya utafiti wa migogoro ya ardhi na kuangalia namna ya kuisuluhisha nje ya mahakama suala ambalo amesema litaokoa  gharama na muda wa wananchi na kuwawezesha kufanya shughuli za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi mahakamani kufuatilia kesi za migogoro hiyo.

Aidha amesema mbali na utafiti chuo hicho kinatoa mafunzo kwa ngazi mbalimbali zikiwemo kozi fupi na ndefu.

“Kozi ndefu tunatoa astashahada ya sheria na stahahada ya sheria na kozi fupi tunatoa kwa watumishi wa mahakama kwa ujumla .

Ndyanabo ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi watembelee banda lao ili wakajifunza Zaidi kuhusiana na shughuli zinazofanywa na chuo hicho.