November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya LG kuja na mkakati mpya kwa wateja wake

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Kampuni ya LG Electronic imejipanaga kuja na mkakati wenye lengo la kujenga ubunifu unaolenga mahitaji ya wateja kwa dhumuni la kujenga maisha bora na kuhakikisha maisha endelevu kwa wote.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa ‘LG World Premiere’ uliyoenda sambamba na Kaulimbiu isemayo “Life is Good”, uliofanyika kando kando ya maonyesho ya CES 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa LG bwana William Cho alisema moja ya mpango mkakati wao wa mwaka 2023 ambao utakua ni endelevu kufikia mwaka 2030 ni kuja na ubunifu mkubwa unaowalenga wateja katika bidhaa zake bora za umeme za majumbani kama vile LG OLED.

“Mpango mkakati wetu uonyesha upatikanaji madhubiti wa uvumbuzi ambao unalenga mahitaji ya wateja kwa dhumuni la kujenga maisha bora kwa kila mmoja, na kujali mazingira, mpango ambao umeambatishwa katika mkakati wa 2023 ESG wenye jina la better Life life, na mpango kazi wake uitwao Better Plan ambao unalenga katika kujenga upatikanaji, urahisi wa bidhaa na huduma kutumiwa na watu wenye walemavu na wazee.” Amesema Cho.

Aidha Cho amesema kampuni hiyo ya LG itachungua changamoto zote mpya katika mwaka 2023 na kuzifanyia kazi ili mteja aweze kupata kitu kilicho bora.

“kampuni ya LG imekuwa inafahamu na kuamini kwa dhati kwamba jibu liko kwa mteja. Mwanzo na mwisho wa ubunifu wote ni wateja wetu, na ni kwa kupitia ubunifu huu ndipo tunapolenga kuweka tabasamu katika nyuso zao.”

Pia Cho alisema kampuni ya LG inampango wa kuongeza upatikanaji na urahisi wa kutumia bidhaa na huduma za LG kwa walemavu na wazee na kuongeza kuwa kampuni inaendelea kutambulisha bidhaa zisizo na uzuizi ambazo zinaweza kutumiwa na watu wote kwa urahisi.

“Dhumuni letu ni kuondoa vizuizi katika hatua zote za matumizi ya mteja. Hatua hii itajumuisha kutengeneza mwongozo wa bidhaa ambao unajumuisha sauti na lugha ya ishara, kusambaza stika za braille kwajili ya watu wenye ulemavu wa macho, na lugha ya ishara kwaajili ya kuendeshea vifaa miongoni mwa mengine.” alisema Cho.

Kadhalika Cho alisema Wataalamu wa LG wanalenga kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 20 katika bidhaa zake 7 kubwa kupitia matumizi yenye ufanisi ya nishati, hata wakati ambapo inalenga kukamilisha mabadiliko yake kuelekea katika nishati mbadala kufikia 2050.

Kwa upande wa sekta ya usafiri Cho alisema kampuni imeungana na baadhi ya makampuni maarufu ya vyombo vya usafiri, kutumia ufahamu wa wateja wake kutoka kwenye watumiaji wa vifaa vya umeme, teknolojia ya kiwango cha juu na maeneo mbalimbali ya utaalamu kuboesha uzoefu wa kusafiri ndani ya gari.

“Hatua hii imepelekea kampuni ya LG kuwa moja kati ya kiwanda cha vifaa vya magari cha kutumainiwa kwa biashara yake ya bidha ya vifaa vya magari, hata wakati ambapo inapanua biashara yake kujumuisha maeneo mapya kama vile chaji za (EV) za magari ya umeme, Vifaa vya kidigitali vya kiafya na huduma ya maudhui kwaajili ya mfumo wa webOS.”

Cho alisema kampuni inaongeza uwekezaji katika teknolojia ya msingi ya siku zijazo, ikiwemo AI na 6G pamoja na kushirikiana na wataalamu chipikizi wa teknolojia kupitia LG, NOVA, (LG North American Innovation Center).

Ikumbukwe kuwa kampuni ya LG imekuja na LG Think UP, ambayo ni aina mpya ya vifaa vya nyumbani vinavyotoa fursa ya kipekee, vinavyoweza kuboreshwa na kubadilishwa kuendana na mahitaji ya mtumiaji ambapo Orodha ya kipekee ya bidhaa zinajumuisha bidhaa za kimapinduzi kama Jokofu la LG lenye MoodUPâ„¢, ambayo inaweza kubadili rangi kuendana na mahitaji ya mtumiaji, anavyojisikia au kuendana na mapambo ya jiko.