November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fahamu visababishi Pumu ya ngozi

Na Mohammed Sharksy

PUMU ya ngozi (Eczem) ni ugonjwa wa ngozi ambao umekuwa ukiwaathiri watoto wengi duniani, Zanzibar ikiwa ni miongoni mwao.

Pumu ya ngozi ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha kuvimba kwa ngozi na kuwa kavu kavu unaoifanya ngozi kuwasha sana na kufanyika kwa vipele vidogo vidogo vyenye rangi nyekundu.

Neno Eczema ambalo ndio jina la maradhi haya kwa kitaalamu ni neno la Kigiriki na linamaanisha kututumka sehemu ya nje ya ngozi, hali ambayo huonekana pale mtoto
anapopata maradhi haya.

Ugonjwa huu wa ngozi unachangia asilimia arobaini ya maradhi yote ya ngozi yanayoripotiwa hospitalini duniani kote.

Chanzo chake ni pale mwili unaposhindwa kutengeneza au kuzalisha chembe hai za mafuta kwenye mwili inayotumika kwenye uzalishaji wa ngozi,chembe hai hizi za mafuta haya inaposhindwa kuzalishwa ngozi hupoteza kiwango cha maji na kuifanya kuwa kavu na mwisho kuanza kuwasha na kujikuna na kuweza kusababisha kujikuna na kubadlika rangi na kuwa nyekundu.

Kama inavyoijeleza hapo juu kwamba waathirika wakubwa ni watoto ,kwa hiyo basi inakisiwa kwamba karibu asilimia 80 ya wagonjwa wenye pumu ya ngozi huanza
kuumwa magonjwa haya wakiwa chini ya umri wa miaka mitano.

Wagonjwa wengi pia huonyesha dalili za maradhi haya wakiwa na umri chini ya mwaka mmoja vilevile ni mara chache sana kuweza kutokezea kwa utu uzima.

VISABISHI VYA PUMU YA NGOZI

Pumu ya ngozi huwa imeambatana na urithi,mabadilliko ya hali ya hewa kama vile kutoka kwenye joto na kwenda kwenye bari au kinyume chake.

Utumiaji holela wa sabuni zinazosababisha kudhurika (allergy) kwa mwili (allegywa mwili,Kukaa kwenye mavumbi mavumbi,Kukaa sana kwenye mchanga,Uvaaji wa nguo hazikutengeneza kwa mali ghafi ya pamba,Kuwa na msongo wa mawazo,utumiaji wa mafuta ya mwili yanayosababisha,kudhurika kwa mwili kwa mwili.

Ulaji wa vakula vinavyo sababisha kudhurika,kama vile kula pweza,dagaa na baadhi ya samaki wa maji ya bahari ya mito au maziwa,Ngozi kukaa kwa muda mrefu bila kuipaka mafuta,Moshi wa sigara na matumizi ya muada mrefu,Mgusano wa kemikali zisizoendana na mwili.

DALILI NA ISHARA ZA PUMU YA NGOZI ZAKE

Dalili kuu tatu wa Pumu ya Ngozi ni ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kupasuka. Pia huambatana na muwasho na kukauka kwa ngozi.

Hii huambatana na magonjwa ya njia ya hewa kama asthma (atopic dermatitis) au baada ya kukutana na kitu kinachosababisha mshituko wa kinga ya mwili na ngozi mfano kipodozi au kemikali nk (contact dermatitis).

Zaidi ya eneo la ngozi kututumka vivimbe pia huweza kuonekana kwenye maeneo ya ngozi yaliyoathirika.Bila matibabu ya haraka ngozi inaweza fanya vidonda.

Ingawa maeneo yenye athari huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini pumu ya ngozi hupenda kushambulia sehemu zifuatazo

PUMU YA NGOZI KWA WATOTO

Asilimia 8 mpaka 18 ya watoto wote uhathiriwa na ugonjwa huu. Hii huambatana na mabadiliko ya hewa na magonjwa ya mfumo wa hewa mfano mafua na asthma. Mara nyingi ugonjwa huu hupotea ukubwani baada ya matibabu.

MATIBABU

Kupata ushauri kutoka daktari juu ya matumizi ya dawa,daktari pia anaweza kutoa dawa ya kupunguza uvimbe ya kupaka kama ataona inafaa.

Daktari pia anaweza kutoa dawa ya kuzuia kinga ya mwili isishambulie ngozi (immunosuppresors drugs), matibabu husika ya ugonjwa wa pumu ya ngozi ni kuondoa uleukavu ukavu kwa kuiweka ngozi na unyevu nyevu.

Matumizi ya dawa za kuondoa muwasho kama vili cetrizen,piriton nakadhalika,Kutumia dawa za cream kwa ajili ya kuzuia mwingiliano ya wadudu wa bakteria,Kuvaa nguo zilizotengenezwa kutumia pamba,kuliko kuvaa nguo za nailoni nakadhalika.

Tibu msongo wa mawazo,oga angalau mara tatu kwa siku ili kuzidi kuilainisha ngozi yako,Tambuwa na kujiepusha vitu vyote vinavyoweza,kupelekea kupata kudhurika kwa pumu ya ngozi kama vile vipodozi feki, jamii ya vyakula vya baharini na vya maji ya bahari nakadhalika,kuogea sabuni isiyo na manukato.