Na Mwandishi wetu
ALIYEKUWA kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Benedict XVI amefariki dunia katika makazi yake Vatican, jijini Roma, nchini Itali
Papa Benedict ambaye aliliongoza kanisa tangu mwaka 2005, alijiuzulu lkwenye nafasi hiyo mwaka 2013 kwa kile kilichoelezwa kupata nafasi ya kuipigania afya yake. Kwa mujibu was taarifa za kuaminika amefariki majira ya asubuhi saa 09:34 akiwa na umri wa miaka 95
Kuhusu kilichosababisha kifo chake, taarifa ya Vatican inasema kuwa Papa Benedict aliugua kwa muda mrefu, lakini bado haijaeleza chanzo cha kifo cha Papa Benedict XVI.
Papa Benedict alizaliwa nchini Ujerumani miaka 95 iliyopita na ndiye Papa aliyevunja rekodi kwa kuteuliwa akiwa na umri mkubwa zaidi, akiwa na umri wa miaka 78 ili kuwa Papa mwaka 2005.
Pia Papa Benedict alipigana Vita ya Pili ya Dunia upande wa Hitle, kisha akawa padri, lakini pia alikuwa ni mkufunzi wa mafundisho ya Mungu aliyekuwa Profesa akiwa na Miaka 31 kisha kuwa Kadinali.
Viongozi mbalimbali wametuma salam kufuatia kifo hicho kati yao akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. katika ukurasa wake wa Twitter, alieleza kusikitishwa kwa kifo cha kiongozi huyo wa dini.
“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedict XVI, ambaye katika Maisha yake katumikia wengine. Natuma salam za pole kwa Baba Mtakatifu Fransisko, waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani kote. Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina,” aliandika Rais Samia.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa