Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika kikao chake cha 189 kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof. Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 96 ya Bodi kwa Watahiniwa waliofanya mitihani mwezi Novemba 2022 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi hiyo ya NBAA.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA. Prof. Sylvia S. Temu amesema kuwa matokeo hayo yameidhinishwa kufuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,429 kati ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani watahiniwa 525 sawa na asilimia 8.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwasababu mbalimbali hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 5,904 sawa na asilimia 91.9 kati ya hao watahiniwa 2,951 sawa na asilimia 49.98 walikuwa Wanawake na watahiniwa 2,953 sawa na asilimia 50.02 walikuwa wanaume.
CPA. Prof. Temu amesema jumla ya watahiniwa 343 wamefaulu mitihani ya Shahada ya Juu ya Uhasibu nchini yaani CPA (T). Kati ya watahiniwa hao wanawake ni 159 sawa na asilimia 46.4 na Wanaume ni 184 sawa na asilimia 53.6. Idadi hii inafanya jumla ya watahiniwa waliofaulu mitahani ya CPA kufikia 12,087 tangu mitihani hiyo ianze mwaka 1975.
Kati ya watahiniwa 343 waliofuzu kutunukiwa Cheti cha Taaluma ya juu ya Uhasibu wengi wao wametoka katika vyuo mbalimbali ambapo watahiniwa 75 sawa na asilimia 21.8 wametoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watahiniwa 48 sawa na asilimia 14.0 wametoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), watahiniwa 27 sawa na asilimia 7.8 wametoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, watahiniwa 23 sawa na asilimia 6.7 wametoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), watahiniwa 16 sawa na asilimia 4.7 wametoka Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).nk
Amesema katika ngazi ya awali ya Uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC I) watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 90 kati ya hao watahiniwa 08 sawa na asilimia 8.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 82 sawa na asilimia 91.1.
Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 82 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 36 ambao ni asilimia 43.9 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku watahiniwa 30 sawa na asilimia 36.6 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii na watahiniwa 16 sawa na asilimia 19.5 hawakufaulu mitihani katika ngazi hii.
Aidha amesema katika hatua ya pili ya Cheti yaani ngazi ya uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC II) waliojisaliwa walikuwa 165 kati ya hao watahiniwa 12 sawa na asilimia 7.3 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 153 sawa na asilimia 92.7.
Pia amesema kati ya watahiniwa 153 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 36 ambao ni asilimia 23.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, watahiniwa 65 sawa na asilimia 42.5 wamefaulu masomo katika ngazi hii na watahiniwa 52 sawa na asilimia 34.0 hawakufaulu mitihani yao katika ngazi hii.
Amesema katika ngazi ya taaluma hatua ya awali watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 776 kati ya hao watahiniwa 73 sawa na asilimia 9.4 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 703 sawa na asilimia 90.6.
Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 703 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 339 ambao ni asilimia 48.2 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku watahiniwa 278 sawa na asilimia 39.5 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 86 sawa na asilimia 12.3 hawakufaulu mitihani yao katika ngazi hii.
Aidha amesema katika hatua ya kati waliojisaliwa walikuwa 3,459 kati ya hao watahiniwa 317 sawa na asilimia 9.2 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa ni 3,142 sawa na asilimia 90.8, kati ya watahiniwa hao 3,142 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 549 sawa na asilimia 17.5 wamefaulu masomo yote katika ngazi hii wengine 1,526 sawa na asilimia 48.6 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 1,067 sawa na asilimia 33.9 hawakufaulu mitihani yao katika ngazi hii.
Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 1,939 kati ya hao watahiniwa 115 sawa na asilimia 5.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 1,824 sawa na asilimia 94.1. Kati ya watahiniwa 1,824 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 344 sawa na asilimia 18.8 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 786 sawa na asilimia 43.2 wamefaulu baadhi ya masomo na watahiniwa 694 sawa na asilimia 38.0 hawakufaulu mitihani yao.
CPA Profesa Temu amesema Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA imetoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.
Pia amesema watahiniwa wote pamoja na wadau wengine kuwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika leo tarehe Desemba 22, 2022 kimepitisha mchakatowa kupitia mitaala ya mafunzo ya Uhasibu hivyo mchakato utaanza mwezi Januari mwaka 2023 na mitaala mipya itaanza rasmi kutumika katika mitihani ya Mei mwaka 2024.
Mitihani ya muhula wa kati pamoja na ile ya Astashahada ya Viwango vya Kiamataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Taasisi za Umma (Diploma in IPSAS) itafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 20 – Ijumaa tarehe 24 Februari mwaka 2023.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â