Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema serikali ina kila sababu ya kuboresha mazingira bora ya vyombo vya habari kutokana na umuhimu wake hasa katika maendeleo na kuinua uchumi wa nchi.
Waziri Nape ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la maendeleo ya sekta ya habari 2022 lilofanyika katika Ukumbi wa Mikiutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaaam.
“Serikali inadhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya habari nchini.””Mwaka 2023 Serikali imekusudia kuongeza nguvu zaidi katika kuboresha maslahi ya wanahabari” Aliongeza Waziri Nape
Waziri Nape amesema Sheria na Kanuni mbalimbali zinaendelea kufanyiwa mabadiliko kwa mujibu wa Sheria lakini pia uhuru wa habari unapaswa kulindwa kwa kujibu wa sheria na siyo utashi wa viongozi.
Pia Nape amesema uhusiano baina ya sekta ya habari na sekta ya umma umeendelea kuimarika katika awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Aidha Waziri Nape amevitaka vyombo vya habari kutimiza wajibu kwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na kulinda lasirimali za nchi.
More Stories
Zaidi ya wananchi 300 wafanyiwa upasuaji wa macho Mbeya
Rais Samia aomboleza kifo cha Papa Francisko
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88