Na Martha Fatael, TimesMajira Online, Moshi
WATANZANIA wametakiwa kuhifadhi raslimali za nchi ikiwemo hifadhi ya mlima Kilimanjaro ambao umekuwa ni kitovu Cha utalii.
Waziri wa maliasili na utalii Dokta Pindi Chana ameyasema hayo mapema hii Leo desemba 5, 2022 Mkoani Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa wapanda mlima Kilimanjaro zaidi ya 200 ambapo nchi mbalimbali zimeshiriki zoezi Hilo, ikiwemo Uganda,uswiz na Sudan na nyingine nyingi ikiwa nikuelkea kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru Tanzania.
Aidha ameonya watanzania ambao wamekuwa wakiharibu hifadhi Kwa kufanya ujangili, kuchoma moto, kukata miti na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na hifadhi hususani vyanzo vya maji ,kuacha mara Moja Kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria Pindi watakapobainika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya hifadhi ya Taifa TANAPA George Waitara amesema serikali imeendelea kuboresha huduma katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro ikiwemo barabara na huduma za afya na zinginezo hivyo kupunguza changamoto kwa wapanda mlima.
Nae mwenyekiti wa mabalozi Dokta Asha Roze Migiro amewahimiza watanzania Kujijegea tabia ya kuutumia utalii wa ndani kwa kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria kujivunia vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba