*Dkt.
Mpango: Sekta Binafasi ichangie zaidi pato la Taifa
*Wanafunzi
ADEM Mwanza wafurika banda la PSSSF
*Viongozi
mbalimbali wafurahishwa na huduma za PSSSF
Na
Mwandishi Wetu, Mwanza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameagiza
sekta ya fedha nchini kuja na ubunifu ambao utaifanya sekta hiyo iweze
kuchangia zaidi katika pato la Taifa.
Dkt.
Mpango alisema hayo Jijini Mwanza katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha
yaliyokutanisha taasisi mbalimbali za fedha ikiwemo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
maadhimisho hayo yalianza Novemba 21, 2022 na yanatarajiwa kufikia tamati
Novemba 26, 2022.
“Kwa
muda mrefu sasa mchango wa sekta ya fedha katika pato la taifa umekuwa chini ya
asilimia nne…hatuna budi kubadilisha mwelekeo huu, ukizingatia jitihada
mbalimbali zilizowekwa hadi sasa, kwahiyo ninaitaka Wizara ya Fedha na Mipango,
pande zote mbili za muungano kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, Umoja
wa Mabenki Tanzania na wadau wote mnaoshiriki maadhimisho haya mfanye tafakuri
ya kina kuhusu namna ya kuongeza ubunifu ili sekta hii iweze kuchangia zaidi
katika jitihada za kupunguza umasikini na kuogeza maendeleo ya
Watanzana”alielekeza Dkt. Mpango.
Katika
hatua nyingine: Wanafunzi wa chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu
(ADEM) tawi la Mwanza wametembelea banda la PSSSF katika maadhimisho ya wiki ya
Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza na kujifunza huduma mbalimbali za
Mfuko ikiwemo huduma ya PSSSF kiganjani.
Idadi
kubwa ya wanafunzi hao walifika katika banda la PSSSF kwa lengo la kufatilia
uwasilishwaji wa makato yao na waajiri wao,hata hivyo baada ya kupatiwa elimu
ya PSSSF kiganjani walivutiwa na wengi wao walielekezwa jinsi ya kutumia huduma
hiyo kupitia simu za kinganjani.
“Kwa
kweli tunawapongeza PSSSF kwa huduma bora, wengi wetu tulifika hapa kwa lengo
la kufatilia michango yetu, lakini baada ya kupatiwa elimu ya PSSSF Kiganjani
tumeielewe na wengi wetu sasa tunaitumia na kuanzia sasa tutakuwa tukipata
taarifa mbalimbali kupitia simu zetu” alifafanua Bw. Shabban Hamza, Wanachuo wa
ADEM.
Huduma
ya PSSSF kinganjani inamwezesha Mwanachama na Mstaafu kupata huduma kupitia
simu janja bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za Mfuko kupata huduma husika.
Huduma zinazopatikana ni pamoja na; Taarifa za uchangiaji, Taarifa za malipo ya
pensheni, Taarifa kuhusu uanachama na kupata mrejesho wa maswali mbalimbali.
Wakati
huohuo: Viongozi mbalimbali watembelea banda la PSSSF katika Wiki ya Huduma za
Fedha na kujifunza mambo mbalimbali, viongozi hao ni pamoja na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango; Mh. Hamad Hassan Chande, Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenerali
Suleiman Mzee, Mkuu wa Wilaya ya Busega
Mhe. Gabriel Zakaria, Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii katika Wizara ya
Kazi, Bw. Festo Fute na Waziri Mstaafu, Mhandisi. Christopher Chiza.
Kwa
nyakati tofauti viongozi hao walifurahishwa na uharaka wa huduma za PSSSF
zinazotolewa katika ofisi zake zilizopo maeneo mbambali ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega Mhe. Gabrieli Zakaria (kulia) akipokea kitabu cha Mwongozo wa Mwanachama
kutoka Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi alipotembelea banda la
PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini
Mwanza.
Waziri Mstaafu,
Mhandisi Christopher Chiza (kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo wa Mwanachama
kutoka kwa Bw. Michael Bujiba, Meneja kutoka kurugenzi ya Fedha ya PSSSF,
alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha
yanayoendelea Jijini Mwanza.
Wanafunzi wa chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) tawi la Mwanza wakiwa katika banda la PSSSF katika maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yanayoendelea Jijini Mwanza, wakielekezwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF kiganjani kutoka kwa Afisa wa PSSSF, Bw. Tabori Mugeta (kushoto).
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi