Na Mwandishi wetu.Songea.
Hemed Challe ameibuka Mshindi baada ya kumbwaga kwa kura 605 Aliyekuwa Mjumbe wa Nec mkoa wa Ruvuma Mussa Homera ambaye alikuwa akitetea nafasi yake na ameambulia kura 52 kati ya 972 zilizopigwa na wajumbe.
Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ,Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mataka amemtangaza Hemed Hamad Challe kuwa mshindi baada ya kupata kura 605 huku wapinzani wake Mussa Homera akipata kura 52 , Daniel Msembele akipata kura 258 na Edwin Millimga kura 30 ambapo wapiga kura ni 972 na kura zilizoharibika 27.
Kwa upande wake mjumbe wa Nec mkoa wa Ruvuma amewataka wanaccm kutulia na kuvunja makundi na kuwa na umoja kwani Uchaguzi limemalizika .
Hemed ameahidi wa CCM kuwa ataendelea kuwawakilisha kwa hekima na upendo.ili kuwaunganisha pamoja wakitumikie chama kuleta maendeleo kwa wananchi
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Wilbert Mahindi amesema mshindi alikuwa na anashahili kushinda kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka pia amekuwa akiwaunganisha wanachama na kuwa wamoja huku akikemea matabaka ndani ya chama.
Naye Cresensia Kapinga ameibuka Mshindi kwenye nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa kupitia CCM wilaya ya songea Mjini kwa kuwa mshindi wa kwanza na kupata kura 486 na kuwabwaga washindani wake wa karibu Luca Ngongi kura 401 ,Mgowole kura 197,West Michael kura 273, Challe kura 160 na CDE Mapunda kura 43.
More Stories
Dkt.Tulia ashiriki ibada, asisitiza waumini kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia