November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashindano ya mpira wa miguu ya maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA yaanza kutimua vumbi

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

KUELEKEA kilele cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameandaa mashindano ya mpira wa miguu yenye jumla ya timu nane na bingwa atafanikiwa kuondoka na kombe, mashindano hayo yameanza tarehe 15-28 Novemba 2022 katika viwanja vya TPDC Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya mpira wa miguu ya Maadhimisho ya miaka 50 ya NBAA yanayoendelea katika viwanja vya TPDC jijini Dar es Salaam Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA CPA Paul Bilabaye amesema kuwa michezo hiyo imekuwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea kilele cha bodi hiyo, na sisi kama sehemu ya watanzania michezo kwetu ni furaha.

“Tunatakiwa kuendelea kusimamia miiko yetu ya uadilifu kwa sababu hiyo ndiyo itafanya taaluma yetu kubaki imara ili kuhakikisha kwamba tufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia uadilifu, cha umuhimu kuheshimu siri tunazopata kutoka kwa wateja wetu ambazo ni siri zao za biashara kwa kuzingatia hayo yataongeza haiba mbele ya jamii” amesema CPA Bilabaye

Aidha, CPA Balibaye ametoa wito kwa wahasibu na wakaguzi nchini kuhakikisha wanafanya mazoezi kutokana wanatumia muda mrefu kukaa ofisini, tujaribu kushiriki michezo ili kuondoa mawazo ambayo huwa tunayapata wakati tukiwa kazini na kuleta tija kwenye jamii zao, hivyo tuendelee kutoa huduma nzuri katika maeneo mbalimbali ya kodi, hesabu.

Hivyo, kwa upande wake nahodha wa timu ya PKF Associates Tanzania Kelvin Christopher amesema wanatumia mashindano hayo kuhakikisha wanatengeneza mahusiano mazuri na wakaguzi wenzao kwa hapa Tanzania na malengo yao kwa PKF ni kuhakikisha wanatoa ubingwa huo.

Naye innovex Auditors Innocent Mageka amesema wao wameshiriki katika mashindano hayo wakiwa miongoni mwa timu nane kubwa ni kufanya mazoezi kwa lengo la kujenga afya kwa sababu muda mrefu sana tunakaa chini zaidi ya masaa 18, pia amewataka wadau mbalimbali kushiriki kwenye michezo kama hiyo.