Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Ukosefu wa mitaji ni moja ya changamoto inayowakabili wanawake wanaofanya shughuli katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini kushindwa kupiga hatua.
Ili kuwainua Taasisi ya kuendeleza wachimbaji wadogo wa madini(FADev), wameanza utekelezaji wa mradi jinsia ambao unatekelezwa kwa wanawake wachimbaji wadogo na wanaofanya shughuli zao za ujasiriamali katika maeneo ya uchimbaji madini.
Meneja Mradi na Utafiti wa Taasisi ya Kuendeleza Uchimbaji Mdogo(FADev),Evans Rubara, amezungumza hayo wakati akizungumza na Timesmajira online jijini Mwanza.
Rubara ameeleza kuwa,FADev kupitia mradi wa jinsia wamejikita kuhakikisha mwanamke mchimbaji mdogo na hata yule anayefanya shughuli za uzalishaji maeneo ya uchimbaji mdogo wanamnyanyua kiuchumi kwa kuwezesha kile wanachokifanya.
“Katika hili tunacho fanya hawa wanawake tunawapatia mafunzo,vifaa kulingana na mahitaji yao,ambapo kikundi cha wanawake wachimbaji Mugusu tumewapa kinu cha kusagia mawe(mbare) pamoja na kiasi cha milioni 6 kama ruzuku ambayo ni mtaji wa kununulia mawe yale sababu mara nyingi wanawake hawaingii maduarani kuchimba,”ameeleza Rubara.
Ameeleza kuwa wanaona mabadiliko makubwa kwa wanawake ambao siyo wachimbaji lakini wanafanya shughuli zao za kijasiriamali katika maeneo ya uchimbaji mdogo wa madini kama wanawake wanaopika chakula(mama ntilie).
Hadi sasa mkoani Geita na Shinyanga wanavikundi 19 vya wanawake wanaofanya ujasiriamali katika maeneo ya uchimbaji mdogo na kati ha hivyo vukundi 12 wamevipatia ruzuku ya milioni 3 ambayo pesa hiyo siyo ya mkopo kusema wanairudisha.
“Fedha hiyo siyo deni bali tunawapa waanze biashara zao ili wajiendeleze na kabla hatujawapatia fedha tunawapatia mafunzo kulingana na mahitaji yao,tunawatengenezea mpango biashara ambao wanaufuata ili kufanya biashara na maisha yao yabadilike,”ameeleza Rubara.
Aidha ameeleza kuwa,wanafanya kazi na vikundi tu mfano kikundi kinafanya au kinahitaji kufanya ujasiriamali wa kutengeneza sabuni wanawapelekea mwalimu na kuwapatia mtaji.
Sanjari na hayo Rubara ameeleza kuwa ili kuweza kuwawezesha wanawake wanaofanya shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na katika maeneo hayo,takwimu ya idadi kamili ya watu wanaojishughulisha katika sekta hiyo inahitajika.
Ambapo takwimu hizo zitabainisha idadi gani wanawake wanafanya shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na kiasi gani wanajishughulisha na shughuli nyingine katika maeneo hayo ya uchimbaji mdogo wa madini.
Hii itasaidia uwezeshaji kwa wanawake na wachimbaji wadogo kwa ujumla kwani kutakuwa na takwimu zenye uhakika na kusaidia wanawake wao Kwa wao kufarakana.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, ameeleza matarajio ya taasisi hiyo katika kuhakikisha mwanamke katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini anasonga mbele aweze kuchangia uchumi na yeye kunufaika kutokana na shughuli hiyo.
Mhandisi Mwasha, ameeleza kuwa nyuma walikuwa wanaona faida zote zinaenda kwa wanaume kwa sababu wapo mbele zaidi katika kuuza,lakini sasa hivi wanatamani mwanamke afaidike zaidi na maliasili hizo popote pale alipo ata kama anapika kwenye maeneo ya madini,ata kama anasogeza mchanga wa mawe ya kwenye dhahabu basi afaidike kama wengine wanaofanya kazi kama hizo anafaidika
“Kusudio letu ni kuona mwanamke anachangia kwenye pato la taifa kwa kufanya kazi pia naye anafaidika kutokana na nguvu zake alizoziweka katika shughuli hizo za uchimbaji mdogo wa madini,”ameeleza Mhandisi Mwasha.
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania