November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Asanteni watumishi wa Afya kwa mlivyojitoa katika ajali ya Ndege-Dkt.Mollel

Na Penina Malundo,timesmajira

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewashukuru Watumishi wa afya wote walijitokeza kuhudumia majeruhi katika ajali ya ndege iliyotokea katika Mkoa wa Kagera iliyotokea Novemba 6, 2022.

Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo leo alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo kwa jitihada za Watumishi wa afya mpaka kufikia leo alibaki majeruhi mmoja tu.

Aidha, Dkt. Mollel amesisitiza Serikali itaendelea kugharamia majeruhi wote waliotokea katika ajali hiyo ya ndege mpaka watakapokuwa sawa kiafya.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiwajulia hali majeruhi wa ajali ya Ndege katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amempongeza Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya za Watanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu kama majengo ya dharura na kuwapa mafunzo Wataalamu ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia katika kuokoa hali ya majeruhi waliokuwa katika ajali ya ndege.