November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Dahua Teknology yaipongeza serikali ya Rais Samia

Na David John timesmajira online

KAMPUNI ya Dhaua Teknoloji inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya ulinzi imesema serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka Mazingira rafiki kwa Wawekezaji hali ambayo imechochea Wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Akizungumza na jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Meneja bidhaa wa Kampuni hiyo Samsoni Ibrahim amesema kuwepo kwa hali ya amani na utulivu nchini imechangia kwa kiasi kikubwa wafanyabishara kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo china kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nakukuza uchumi wa Tanzania.

” Napenda kushukuru Serikali ya Tanzania na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa Kutuongozea nchi yetu kwa kutuwekea mazingira ya amani na hata wawekezaji hao wanaokuja wanakuta mazingira yako vizuri hivyo inatupelekea hata sisi kupata fursa ya kufanya kazi na nchi mbalimbali,hivyo ni jambo zuri sana linalofanywa na serikali ya awamu ya sita,amesema Ibrahim.

Ameongeza kuwa Kampuni ya Dahua Teknology yenye makao yake Makuu nchini china inazalisha vifaa vya kusimamia usalama wa watu na mali zao kama vile Magari,pamoja na kudhibiti vitendo vya uhalifu kwani uhalifu mwingi unafanyika kwa kutumia usafiri wa Magari na Pikipiki.

“Vifaa tulivyo navyo siyo kwa ajili ya kudhibiti usalama wa watu na mali zao pakee lakini pia tuna vifaa aina nyingi ikiwemo vifaa vya kufuatilia data muhimu kwa serikali,kampuni binafsi hata Benki wanapotaka kupata data mbalimbali za kibiashara,tunateknolojia za kisasa aina zote zinazofaa kwenye ulinzi lakini pia usalama wa biashara( Business Intelligence) amesisitiza

Nakuongeza kuwa” pia tuna vifaa vya kuwezesha kufanya mikutano kwa njia ya mitandao ( Video Conference) pamoja na vifaa aina ya Droni zinazotumika kurekodi picha za matukio angani,hivyo ameziomba taasisi mbalimbali kutembelea sehemu yao ya kuuzia bidhaa zao katika Maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam.