Na David John,timesmajira, Online
SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na michezo imedhamiria kuinua sekta ya sanaa hapa nchini kwa kuwaunganisha wasanii wa Tanzania na wasanii wa Afrika ili kuweza kukuza uwezo na ufanisi wa kazi zao
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo. Dkt. Hassan Abass alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JuliusNyerere JNICC.
Dkt Abass amewaeleza wanahabari kuwa wameandaa tamasha kubwa nchini ambalo linakwenda kuwakutanisha wanamuziki wa bara la Afrika na Tanzania.
Amesema tamasha hilo linatarajiwa kuanza Novemba 24 hadi 26 mwaka huu na linatarajia kuwapa fursa wanamuziki wa Tanzania kukutana na wanamuziki wengine wa ngazi ya kimataifa kuweza kubadilishana ujuzi na kukua kibiashara.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu washirikisho la wasanii hapa nchini msanii Faridi Kubanda (FidQ) aliwataka wasanii kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani kujiandikisha hakuna gharama yoyote na hiyo ni fursa kwa wasanii wa Tanzania kukutanishwa na wanamuziki wa ngazi ya kimataifa.
Amesema wanawashukuru walioandaa tamasha hilo ACCES Music in Afrika kwani tamasha litawawezesha wasanii kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza elimu katika sekta ya muziki.
“Tamasha litawawezesha wasanii kukutana wa wasanii tofauti kutoka nje na kutawawezesha hata kufanya nao kollabo za kimataifa, ikiwemo na kuvumbua vipaji kwenye sekta hiyo ya Muziki.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa