Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wauguzi na wakunga waaswa kuwa na lugha nzuri na ubunifu wa hali ya juu katika kuwahudumia wagonjwa Hospitalini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bi. Ziada Sellah katika kikao na wawakilishi wa wauguzi na wakunga kutoka katika wilaya za Msalala, Ushetu na Kahama Mkoani Shinyanga kujadili changamoto mbalimbali katika kada hiyo.
“Fanyeni kazi ya uuguzi na ukunga kwa moyo wote, kumekuwa hakuna kauli nzuri kwa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wetu wetu pindi wanapokuja katika Hospitali zetu” amesema Bi. Ziada.
“Wauguzi na wakunga wenzangu tubadilike, lugha kwa wagonjwa ikiwa nzuri kila mtu ata tamani kuja kutibiwa katika hospitali zetu ” Amesema Bi. Sellah
Ameendelea kusema Wauguzi na Wakunga wanahitaji kuwapa faraja wagonjwa na wateja wetu ili kuboresha huduma katika vituo vyao.
“Twendeni tukaboreshe huduma kwa kadri tulivyo fundishwa kwa kufuata kanuni taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya ikiwa ni kuwapa faraja wagonjwa wetu ” Amesema Bi. Sellah
Aidha Bi. Sellah amewasihi wauguzi na wakunga kuwa wabunifu katika kuwahudumia wagonjwa
“Unapokuwa mbunifu kwenye kumhudumia mgonjwa itasaidia kuongeza utoaji wa huduma bora katika vituo vyetu na kuwavutia wagonjwa wengi kuja Hospitalini” Amesema Bi. Sellah
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa