November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Agri-Connect kuongeza kipato kwa wanawake na vijana

Na David John, TimesMajira Online

MTAALAMU wa Mawasiliano wa Mradi wa Agri-Connect Michael Neligwa amesema kuwa Agri-Connect ni mradi ambao upo chini ya Wizara ya Kilimo na unafadhiliwa na umoja wa nchi za Ulaya na ni mradi ambao unagharimu shilingi za Kitanzania zaidi ya bilioni 270 na lengo lake kubwa ni kusaidia kilimo cha mazao ya Kahawa,Chai,pamoja na mbogamboga.

Amesema kuwa pia mradi huo umejikita kwenye maeneo ya lishe ikiwemo na kuwashikirikisha vijana pamoja na wanawake kwa lengo la kuongeza kipato chao cha kiuchumi,kushiriki kwenye shughuli za kilimo kwa ujumla lakini pia kupambana na mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Michael aliyasema hayo hivi karibuni kwenye maonyesho ya Chakula na lishe ambayo yalifanyika mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Halmashauri ya Bariadi ambapo pia alisema maeneo mengine ambayo wanashughulika nayo kupitia mradi huo ni kutunza Mazingir,kuwezesha kuondoa vikwazo vinavyojitokeza na kukwamisha uwekezaji kwenye sekta ya kilimo vinaondolewa.

Pia alisema kuwa Mradi huo unahakikisha mazingira ya biashara yanaimalika na vilevile kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo na kuweza kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo wa thamani kwenye mazao ya kahawa,chai,pamoja na mboga mboga na matunda.

“Agri-Connect Tunashirikiana na taasisi mbalimbali ambazo kimsingi zinatekeleza kile ambacho mradi umekusudia taasisi hizi zinashirikishi moja kwa moja ngazi ya chini ambako mkulima yupo,shirika la Helvetas,IDH,RIKOLTO,SOLIDARIDAD,VI AGROFORESTSTRY,TRIAS,PDF pamoja na shirika la chakula la umoja wa Mataifa FAO”alisema

Aliongeza kuwa miradi hiyo inatekelezwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Zanzibar,katika mikoa ya Katavi,Songwe,Mbeya,Iringa,Njombe,Ruvuma pamoja Unguja na Pemba Visiwani Zanzibar.

Michael alisema pia mradi umejikita na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya lishe,uchakataji wa mazao ili kufikia kwenye viwango bora na kufikia masoko ya nje na kutumia mbinu mbadala kwenye uzalishaji ambapo kuna mashine ambazo ni rahisi zinazoweza kuwasaidia wakulima na kujua ninamna gani kufanya shughuli za kilimo kwa kutumia teknolojia rahisi.

Alifafanua kuwa ushiriki wao katika maonyesho ya Chakula na lishe kumewezesha kutoa fursa ya kuonyesha umma kwa ujumla kuhusu wanavyoweza kutumia teknolojia rahisi zinazoweza kupataka kwenye maeneo yao huku akitolea mfano pembeje pamoja na viwatilifu ambavyo kimsingi vinakuwa ni mbadala wa viwatilifu vinavyopatikana maduni au kiwandani hivyo hizo ni malighafi ambazo zinapatikana kwenye maeneo yao na ili kuweza kuimalisha kilimo wanachokifanya.

Akizungumzia eneo kubwa ambalo asiliamia 48 ya gharama ya mradi zimepelekwa kwenye kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabara vijijini inaimalika na miundombinu hiyo ya barabara imejengwa kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini kwenye mikoa ya Iringa na Njombe ambayo inatekelezwa kikamilifu na Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA) ambapo barabara zenye urefu takribani 350 zimejengwa.

Alisema kuwa na barabara hizo kimsingi zimelenga kuweza kuwasaidia wakulima kwalengo la kuondoa upotevu wa mazao lakini pia kuwarahisishia wakulima ili kuweza kuyafikia masoko kwa urahisi na kuwasaidia wakulima kuyafikia maeneo ambayo yanafanya uchakataji wa mazao kwa mfano mbogamboga na matunda.usafirishaji wa mazao mengine.

Alisisitiza kuwa mradi huo wanashirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo ambao hajaweza kuwataja lakini pia sekta binafsi ambayo kimsingi inalengwa sana na mradi huo na kuangalia mazingira ya uwekezaji yanaimalishwa na kushiriki kwenye ufanyaji wa biashara na urahisi wa kufanya biashara uweze kuwa mzuri na hiyo ni jitihada ya kuunga juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amejipambanua kuwa uwekezaji unaimalika kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.

Mtaalam wa Mawasiliano wa Mradi wa Agri -Connect akizungunzia kazi zinazofanywa na shirika lao mbele ya waandishi wa habari. (Hawapo pichani)