November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkoa wa Ruvuma waongoza kitaifa kwa kutoa chanjo ya Uviko-19 kitaifa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Tangu kuzinduliwa kwa chanjo ya UVIKO-19 na Rais Samia Hassan mnamo Julai 2021, na baadae kufuatiwa na kampeini nchi kote kuhusu chanjo, Wizara ya Afya ilikuwa na lengo la Kujanja Watanzania kwa asilimia 70 mpaka mwisho wa mwaka huu kwa kushirikiana na wafadhili pamoja na wadau wa maendeleo.

Wizara ya Afya ilikuja na mbinu tofauti za kuhamashisha wananchi kujitokeza ili kupata chanjo.

Baadhi ya mbinu ni kuwatumia wanasiasa, viongozi wa vijiji na viongozi wa dini, kutumia watoa huduma wa afya ndani ya jamii. Mbinu hizi ziliiwesha Mkoa wa Ruvuma kuweza kufikia lengo la taifa la Kujanja zaidi ya asilimia 70 ya wananchi kabla hata mwaka kumalizika.

Na ili kuweza kuendelea kutoa chanjo ya UVIKO-19 na hatimaye kufikia asilimia 100, kampeini ya kuhamashisha na kutoa elimu juu ya chanjo yenye kauli mbiu Mziki Mnene Ujanja Kujanja ilizinduliwa mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki huku akiongozwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo Marioo, Snura, Ney wa Mitengo, Stamina, Mr Blue, ManFongo, Jay Melody, Baddest 47 na Tunda Man.

Tamasha hili lilifanyika kwenye viwanjwa vya Maji Maji mjini Songea na iliandaliwa na na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha Elimu kwa Umma, pamoja na FHI 360 kupitia mradi wa EpiC kwa ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Wizara ya Afya kupitia kitengo cha Elimu kwa Umma imekuwa ikitumia matamasha ya muziki kutoa elimu na kuhamashisha jamii juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO-19. Mpaka kufikia sasa, matamasha hayo yameweza kufanyika kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara ra Ruvuma.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Louis Chomboko alisema kuwa mkoa wa Ruvuma kwa sasa umeweza kuvuka lengo la taifa la kutoa chanjo kwa asilimia 70.

“Lengo la taifa ni kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi wake kwa asilimia 70 kabla ya mwisho wa 2022. Naomba nichukue fursa hii kusema kuwa sisi Mkoa wa Ruvuma tayari tushavuka lengo hili.”

“Haya ni mafanikio makubwa kwa kuwa mkoa wetu unapakana nan chi jirani wetu nah ii inaonyesha ni kwa jinsi ngani tumejitolea kuwakinga wananchi wetu.”

Chomboko aliongeza, Nachukua fursa hii kushukuru Wizara ya Afya, viongozi wa kitaifa, USAID pamoja na wadau wetu FHI 360 kupitia mradi wa EpiC kwa kuhakikisha kuwa inapatikana muda wote, lakini zaidi ni kwa kutoa elimu na kuhamashisha jamii yetu juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO-19.

“Naomba kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuweka nguvu kwenye kampeini hii ili kila mwananchi ambaye anastahili kupata chanjo anapata kwa ukaribu kwenye hospitali zetu za umma, kwenye vituo vya afya pamoja na maeneo mengine ambayo yameruhusiwa kutoa chanjo kwa kufuata taratibu zikizowekwa na serikali.”

Kampeini ya chanjo ya UVIKO-19 ambayo inaratibiwa na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha elimu wa umma pamoja na wadau FHI 360 kwa ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kauli mbiu Bega kwa Bega, Ujanja Kujanja itaendelea kwenye mikoa ya Njombe na Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Laban Thomas alitoa pongezi kwa viongozi wa afya wa mkoa kwa kuweka nguvu na kufanikisha lengo la taifa la kutoa chanjo.

“Kwa kuwa mkoa wa kwanza kufikisha lengo hili la taifa, inaonyesha ni kwa jinsi ngani mumejitolea kusaidia wananchi wetu. Kwa kutumia njia zenu wenyewe kufikisha lengo na sasa kwa kutumia tamasha hili la muziki ambalo limeweza kuvuta umati mkubwa wa wananchi, nina uhakika mtaendelea kufanya vizuri zaidi.”

EpiC ni mradi wa kimataifa wa miaka mitano unaotekelezwa na shirika la FHI360 kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), uliojikita katika kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ni kupitia kutoa msaada wa kitaalamu na huduma za moja kwa moja katika kuondoa vikwazo vilivyopo kufikia 95-95-95, na kuhamasisha usimamizi wa kujitegemea wa miradi ya VVU/UKIMWI kitaifa kwa kuboresha programu za utambuzi wa hali ya maambukizi ya VVU, kinga, matunzo na tiba.