Na Penina Malundo, timesmajira,Online
OFISA Utalii wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Muhogolo Joshua amesema ni muhimu kwa wasanii mbalimbali nchini kuhakikisha wanatumia kazi zao za sanaa kuelimisha jamii kuhusiana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo yameanza kujitokeza.
Joshua ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija katika ufunguzi wa maonesho ya wasanii wa uchoraji picha yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi (GCCTC).
Amesema wasanii watakapotumia sanaa zao kuelimisha jamii kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira zitasaidia kwa kiasi kikubwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake kuchukua hatua ya kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Pia tunatoa wito kwa wanafunzi waliopo vyuoni na vijana majumbani kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuanzisha vikundi mbalimbali vya upandaji miti na vitakavyokuwa vikitoa elimu kwa jamii,” amesema JoshuaÂ
Aidha Joshua amewashukuru wasanii wote walioshiriki katika maonesho hayo kwani wameweza kueleza kwa kupitia sana ya uchoraji juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Â
“Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuunga mkono jitihada hizi za wasanii wetu wachoraji kwa kujitokeza kuwasapoti kwa hali na mali ili kuendeleza kazi zao, kwani mabadiliko ya tabianchi yapo na yameanza kuleta athari nyingi duniani na Tanzania ikiwemo,” amesemaÂ
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuhimiza na kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira kupitia njia mbalimbali ikiwemo njia ya sanaa na watu kuelewa na kuchukua hatua stahiki.
Naye Mratibu wa Mtandao wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi (GCCTC), Maria Matui amesema wameweza kutoa mafunzo kwa wachoraji 15 ambayo yanalengo la kuwezesha kutoa ufahamu kwao na kwa jamii kuhusiana na mkakati wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2021/2026 uliyotolewa mwaka jana na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Amesema njia moja wapo ambayo waliitambua kuwa inaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ni kutumia sanaa za michoro mbalimbali na kwamba watendelea kutoa elimu hiyo na kuchagiza vijana kushiriki kwa wingi katika maonesho hayo.
Naye Mwenyekiti wa GCCTC, Marcela Lungu alisema mtandao huo utatumia sanaa yeyote ile ambayo itaweza kuwavuta vijana wakiwemo wasanii kuwaelimisha jamii kuhusiana na mabadiliko hayo ya tabianchi.Â
“Tumeanza na sanaa ya uchoraji, tutakuja kwenye muziki, maonesho ya mavazi, ngoma na nyingine nyingi, lengo letu tunataka kundi kubwa la vijana na wanawake kushiriki ipasavyo katika mabadiliko haya ya tabianchi,” amesemaÂ
Aidha Mmoja wa wachoraji katika manesho hayo, Christopher Nyiti amesema wanaendelea kutumia sanaa yao kuelimisha jamii juu ya kuzuia uharibifu wa mazingira ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko hao ya tabianchi.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili