November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kanali Ngata: Maonesho ya nane nane yatatoa fursa kwa wakulima wa mazao

Na David John Timesmajira online Mbeya

MKURUGENZI Mtendaji wa suma JKT Kanali Petro Ngata amesema kuwa anauhakika baada ya kumalizika kwa maonesho ya Nane Nane ya wakulima watakuwa wamepata maarifa ya namna bora ya kuzalisha mazao.

Kanali Ngata ameyasema haya leo Agosti 2 Jijini Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nane nane yaliyofunguliwa Agosti mosi mkoani humo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Amesema kuwa wakulima hao kwa kiasi kubwa watakuwa wamepata mafunzo ambayo yatakwenda kuwasadia katika shughuli zao za kilimo katika maeneo yao.

Akizungumzia ongezeko la bajeti katika wizara ya kilimo Kanali Ngata amesema bajeti hiyo italeta tija kubwa sana kwa kilimo kwa kila mtanzania kwasababu unamaana serikali itatanua na kuweka mkazo mkubwa sana kwenye sekta ya kilimo hususani kwenye pembejeo.

Ameongeza Kuwa anauhakika kwa bajeti hiyo kubwa ambayo imeongezwa italeta uzalishaji mkubwa na wao kama jeshi wamejipanga vizuri na wanamashamba makubwa Nchini na wameaza mikakati ya uzalisha mkubwa hasa kwenye mazao ya Mahindi ,Mpunga na zao la mazao ya mafuta .

Kanali amesema lengo ni kuondoa tatizo la mafuta ambalo lipo hivyo anawakaribisha wananchi wote kwenye eneo la jeshi la kujenga taifa ili waende wakajifunze kwani wanawatalamu wazoefu kwenye eneo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Maonesho ya Nane Nane kitaifa kutoka Suma Jkt Kanali Shija Lupi akizungumza kwenye maonyesho hayo amesema kupitia kauli mbiu ya maonesho hayo inayosema Sensa Kilimo ni Biashara Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi amewataka wananchi wote kufika kwenye banda la jeshi la kujenga taifa kujionea bidhaa nyingi za kilimo na uvuvi.

Amesema kuwa kuna sehemu mzuri ambayo wanafundisha wakulima jinsi ya kupanda na kulima mazao mbalimbali kama mahindi lakini pia wanafundisha namna bora ya uvuvi na mengineyo kwani wanawatalamu wengi sana hivyo wafike viwanja hivyo vya nane nane

Naye Mkurugenzi wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi kanali Peter lushika amesema kuwa wao jukumu kubwa nikutoa elimu kwa wafugaji ,wakulima na wavuvi hivyo kwa upande wa sekta hizo wanatoa elimu juu ya ufugaji kwani wamekuja na utaalamu wakufuga samaki kwa njia ya mabwawa.

Amesema kuwa wanafuga samaki kwa njia ya vizimba lengo nikuona sekta hiyo inaweza kutumika maeneo yote mjini na vijijini na utaalamu mwingine ni kwa njia ya mabwawa ambapo lengo wafuge samaki na wapate samaki bora zitakazokwenda kutengeneza afya bora kwa watu.

Ameongeza kuwa ufugaji wa samaki unamchango mkubwa na katika ufugaji wa samaki hilo ndio eneo kubwa la uchumi wa bahari na kwamba na katika upande wa nyanda za juu kidini hususani mkoa wa Mbeya changamoto kubwa ya eneo ni baridi sana hivyo inaleta changamoto kidogo katika upande wa ufugaji samaki na ndio maana wanatoa mafunzo ya ufugaji ili wafuge vizuri.