Na Cresensia Kapinga, TimesMajira Online, Songea
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ruvuma (TAKUKURU) imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 yenye thamani ya jumla ya sh. Bilioni 5 .9.
Katika ufuatiliaji huo TAKUKURU imebaini ucheleweshwaji wa malipo kwa wakandarasi ambao pia unapelekea kucheleweshwa kwa kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa, inatekelezwa kwa wakati ikiwa na ubora na kulingana na thamani ya fedha zinazotolewa.
Kamanda Mwenda ameitaja miradi hiyo iliyofuatiliwa kuwa ni ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya maji katika vijiji na kata mbalimbali yenye thamani ya sh. Bbilioni 4.8, ujenzi wa nyumba moja ya watumishi yenye thamani ya sh. milioni 90 ujenzi na ukarabati wa barabara katika misitu ya hifadhi yenye thamani ya sh. mMilioni 6 .9 , ujenzi wa jengo la huduma za dharura kwa thamani ya sh. milioni 3 na ujenzi wa geti katika msitu wa asili wa Matogoro lenye thamani ya sh. Milioni 60.
Aidha Kamanda Mwenda amesema kuwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2022 TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma ilipokea taarifa 44 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali na malalamiko yote yalifanyiwa kazi Kati ya malalamiko 44 taarifa 19 zilihusu rushwa na uchunguzi wake bado unaendelea malalamiko 25 haya kuhusu Rushwa.
Hata hivyo amesema kuwa katika kipindi hiki wameweza kufungua kesi mpya tatu na kufanya jumla ya kesi zilizoendelea mahakamani kuwa kesi tisa, , kesi zilizoamuliwa mahakamani katika kipindi hicho ni nne, ambapo kati ya hizo Jamuhuri imeshinda keai mbili na kushindwa kesi mbili.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili