Na Penina Malundo,timesmajira, Online
UNYWAJI wa Pombe na miundombinu hafifu ya wavuvi wanayovulia samaki ikiwemo vyombo wanavyoendesha baharini vmeelezwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali za baharini zinasababisha wavuvi wengi kufariki duniani na wengine kupata majeraha ya kudumu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Tawala wa Manispaa ya Kinondoni,Stella Msofe wakati wa maadhimisho ya siku ya Kuzuia Kuzama Duniani iliyoandaliwa na Shirika la Mazingira na Maendeleo Tanzania (EMEDO)kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Amesema kwa sasa wavuvi wanapaswa kuacha tabia za mazoea kuingia baharini huku wakiwa wamelewa na kuingia na vyombo vibovu vya uvuaji wa samaki kwa kufanya hivyo kutaweza kusaidia kuokoa maisha yao wakiwa katikia shughuli za uvuvi.
Msofe alisema ni muda sasa wa wavuvi kuamka na kuamua kusonga mbele kuacha tabia zote zinazopelekea kuhatarisha maisha yo wawapo baharini.”Tusikubali kwa namna yoyote kufanya vitendo ambavyo vinaweza kupeleke nyie wavuvi kuwa katika hali ya hatari ya moja kwa moja kuweza kuzama.”amesema na kuongeza
”Sasa mnapaswa kuchukua  hatua katika kuhakikisha  kuwa walinzi wenyewe  ili mnapoingia ndani ya bahari kujiandaa na kujilinda katika shughuli zote za uvuvi  ili endapo hatarini inapotokea kuweza kuchukua hatua za kujiokoa,”amesema
Aidha amesema katika maadhimisho hayo ya siku kuzuia kuzama baharini ,wavuvi wanatakiwa kuendelea kupatiwa elimu mbalimbali za kujizuia kuzama na namna ya kuokoa wenzao endapo wanapopata majanga ndani ya bahari.
”Tunapoelekea kupunguza vifo hivi na kuviondoa kabisa ni kuhakikisha wadau mnaendelea kutoa elimu kwa wavuvi za kuwasaidia kuzuia kuzama na kupoteza maisha ndani ya bahari na kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa usalama,”amesema
Kwa Upande wake Ofisa Elekezi wa Shirika la EMEDO,Grace Andrew amesema ukubwa wa tatizo la vifo vinavyotokana na kuzama maji duniani umethibitishwa na tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Amesema Shirika la afya duniani(WHO)linakadiria kuwa 236,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuzama maji.”Miongoni mwa makundi yanayoathirika zaidi na tatizo hili ni wavuvi pamoja na watoto pia madhara ya kijamii na kiuchumi kwa familia husika ni makubwa,”amesema na kuongeza
”Shirika la EMEDO kwa kuona hilo limeweza kuadhimisha siku hii huku ikiwapatia wamama wa msasani viatu maalum vya kuingilia baharini na glopsi kwaajili ya kuchokoa  chaza baharini,”amesema
Naye Mkufunzi wa Mafunzo wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Kampasi ya Mbegani(FETA)Kapten, Nicas Mbandi amesema mwaka 2017 hadi 2019 walifanya tafiti wakitumia boti ya kumulika waligundua kuwa kati ya wavuvi 40 kati ya 25 wanakuwa wamelewa pindi wanapoingia baharini kwenda kuvua samaki.
”Kazi za bahari ni ngumu sasa mtu anapofikilia kuwa anaingia baharini huku amelewa anakuwa amepunguza baadhi ya msongo wa mawazo kumbe inakuwa ni hatari zaidi kwao,”amesema
Aidha Mwakilishi wa Wavuvi wa Mwalo wa Msasani,Swaumu Hamza amelisema Serikali kutazama tatizo la vifo vya wavuvi vinavyotokana na kuzama maji kwa jicho la kipekee kwani kwa manispaa ya kinondoni kwa wastani kila mwezi vifo visivyopungua watu watano wanaozama baharini.
”Changamoto ya kuzama kwa wavuvi ni kubwa kwa ukanda wa baharini hasa katika kipindi hiki cha upepo mkali,tumekuwa tukishuhudia wavuvi wenzetu wakipoteza maisha kila siku kwa sababu ya uduni wa vyombo tunavyotumia kuvua samaki,baadhi ya wavuvi kwenda baharini wakiwa wamelewa pamoja na Ukosefu wa elimu juu ya mbinu za kujiokoa,”amesema na kuongeza
”Tunaamini serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweza kulingalia hili ili kusaidia ajali hizi kupungua huku bei za vifaa vya usalama kwenye maji nayo viweze kupungua bei ili wavuvi na wamiliki wa vyombo waweza kuzimudu,”amesema
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi