Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda amesema mfumo wa kidigitali ndio utakaotumika kukusanya taarifa za watanzania tofauti na mfumo wa kianalogia uliokuwa ukitumika kukusanya taarifa mwaka 1967 lilipofanyika zoezi hilo kwa awamu ya kwanza.
Kamisaa Makinda ameyasema hayo katika Mkutano wa viongozi wa dini, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi pamoja na makatibu tawala kuhusu maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uliofanyika jijini Tanga ambapo Kamisaa Makinda amesema wanatarajia katika zoezi hilo kila mtanzania atahesabiwa kwa maslahi ya Taifa.
Kamisaa Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika mkutano huo amewaagiza viongozi wa dini na kimila kwenda kutumia majukwaa yao na nyumba za ibada kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu zoezi hilo la kitaifa itakapofika Aguost 23, 2022.
“Lengo la serikali katika Sensa ya mwaka huu ni kuhakikisha tunapata takwimu sahihi kusudi iweze kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kulingana na uhitaji mazingira yaliyopo hivyo ni takwimu tulizonazo hatutaki ziishie kwenye vitabu tunataka zishuke hadi kwa wananchi wa hali ya chini ili tuweze kujua pia uchumi wetu umekuwa kwa kiasi ganu” alisema Makinda.
Aidha Makinda alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inapata takwimu za wafanyabiashara wadogowadogo maarufu Kama wamachinga ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi ambapo limeandaliwa dodoso rasmi kwaajili yao ili kuweza kuwatambua kwa idadi.
“Katika Sensa hii ya mwaka 2022 kutakuwa na dodoso maalumu la wamachinga ili kuweza kuwatambua watakuwa na kadi za kudumu hivyo ni kitu ambacho kitasaidia sana pamoja na serikali yetu” alisema Makinda.
” Kazi ambayo ipo kwetu sisi wote ni kuelimisha na kuhamasisha lakini bila viongozi wa dini na kimila hatuwezi kufanya kazi peke yetu hivyo viongozi wa dini tunawaona Kama ni watu ambao wanasikilizwa na jamii tungekuwa tukiwatumia kila mara na tunaamini watatusaidia ” aliongeza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amesema zoezi hilo lina manufaa makubwa kwa Taifa na kutaka jamii kujitokeza na kuhesabiwa.
Malima alisema kuwa wamejipanga pamoja na kamati za mkoa wilaya na viongozi wote kuhakikisha kuwa Tanga inakuwa msatari wa mbele kufanikisha Zoezi hilo kwa ngazi ya kitaifa.
“Licha ya kuwa mkoa wa atanga no mkubwa kiutawala lakini tunaamini kuwa tutahakikisha na tumejipanga kuwa wa kwanza kufanikisha Zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 na hii tumejipanga kufanya vikao na viongozi wa dini wa mila pamoja na kamati za senza katika Tanga hii Mimi nikiwa ni mkuu wa mkoa naomba mtambue kuwa nimeweka maendeleo’ mbele”
” Tutahakikisha kuwa viongozi wa dini wanafikisha ujumbe kwa waumini na Wananchi wote kwa ujumla nikiamini zaidi kuwa katika kufanikisha hili viongozi wote wa dini mnayi nafasi katika kufanikisha Zoezi hili la kitaifa”
Aidha Malima ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga alibainisha kuwa hatomvumilia mtu au kikundi chochote Cha watu watakaojaribu na kutaka kukwamisha kufanikisha Zoezi la Sensa ya watu na makazi badala watakutana na mkono wa sheria.
“Pamoja na sura ya uelimishaji na uhamasishaji pale ambapo tutakuta Kuna mtu au watu wanaoenda kinyume au kupotosha suala hili la Sensa ya watu na makazi tutamshughulikia kisheria , mimi agenda yangu nikiwa ni mkuu wa mkoa wa Tanga ni kuhakikisha maendeleo’ ya mkoa yanapatikana “
Awali akitoa taarifa ya maandalizi ya Sensa mtaalamu wa habari na mawasiliano kutoka ofisi Taifa ya Takwimu Said Ameir alisema kuwa Sensa ya mwaka 2022 ambayo ni ya sita hapa nchini kufanyika itafanyika tofauti na awamu zote ambapo karani atarekodi taatifa za kila kaya kupitia simu janja ambapo takwimu zitakuwa zinapatikana katika kila kitongoji kwa kila eneo husika.
” Hii itatusaidia kukusanya taarifa za takwimu na kujua ni wapi panahitaji huduma gani Jambo kubwa ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatoa taatifa sahihi kwa makarani, kabla ya Sensa karani atatembelea eneo lake la kuhesabia kwa lengo la kujua na kutambua ni huduma gani za kijamii zinapatikana kwa kushirikiana na viongozi wa eneo husika” alisema Am
Viongozi wa dini wameahidi kutumia majukwaa yao kuhamasisha jamii dhidi ya zoezi hilo kwa muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Zoezi hilo la sensa ya watu na makazi linatarajiwa kufanyika agosti 23 mwaka huu na linafanyika ikiwa ni awamu ya sita tokea zoezi la sensa kufanyika mwaka 1967 kwa mara ya kwanza.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi