Na Hadija Bagasha Tanga,
Waziri wa Nchi anayeshughulikia maendeleo ya madini kutoka wizara ya nishati na madini Nchini Uganda Peter Lokeris amesema wanaangalia namna ya kutumia bandari ya Tanga kupitia kampuni ya GBP kuagiza mafuta yao yatakayoweza kusafirishwa kwa njia ya barabara au reli.
Waziri huyo ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea kampuni ya mafuta ya GBP iliyopo jijini Tanga ikiwa ni baadhi ya miradi waliyoitembelea kwenye ziara yao Nchini Tanzania.
Waziri Lokeris amesema waamini hatua hiyo itasaidia kurahisisha kwenye uingizaji wa mafuta tofauti na njia wanayoitumia kwa sasa.
Aidha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia pia kwasababu wao pia wanazalisha bidhaa nyingi hivyo itawawezesha na wao kusafirisha bidhaa zingine kutoka nchini Uganda na kuja Tanzania.
Amesema hatua hiyo inatajwa kuimarisha mahusiano kati ya Nchi hizo mbili huku akiitaka kampuni ya GBP kuwekeza Nchini Uganda.
“Kwanza kabisa niipongeze kampuni ya GBP kwa namna walivyowekeza Nchini Tanzania huu ni mfano wa makampuni mengine kuiga sisi Unganda tunakaribisha sana GBP kuja kuwekeza tukiahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwenye uwekezaji wao, “alisema Waziri huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya GBP Badar Sood amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha sekta binafsi kuwekeza bila vikwazo vyovyote na jambo ambalo limekuwa likileta maendeleo ya Nchi hali inayopelekea kuongezeka kwa wageni wengi kutoka nje ya nchi.
“Tumepokea ugeni huu kutoka Nchini Uganda pamoja na viongozi wetu wa wizara ya Nchini wakiongozwa na katibu mkuu Mramba kimsingi tunashukuru kwa pongezi ambazo wametupatia kwajili ya uwekezaji hapa hivyo tunawakaribisha kuwekeza kufanya biashara kwa pamoja kwakweli wameridhishwa na wapo tayari kutumia GBP Tanga Terminal kwajili ya upokeaji wa mafuta ya kwenda Uganda ambayo yatasafirishwa kwa njia ya meli, reli au barabara “alibainisha Badar.
Aidha aliishukuru serikali ya Uganda kwa kuwakaribisha kwenda kuwekeza Nchini humo na kueleza kuwa wanategema kufanya biashara kwa maslahi ya pande zote mbili.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati Dastan Kitandula alisema kuwa ujio huo una mafanikio na manufaa makubwa kama inavyofahamika nchi hizo mbili zimeingia kwenye makubaliano ya kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka nchini Uganda kuja Chongoleani Tanga ili kuwawezesha wadau kuuza mafuta yao nje ya bara lao.
“Kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni ya uwekezaji mkubwa ambao unatarajiwa kuleta manufaa kwa Tanzania na wenzetu wa Uganda lakini kama mnavyofahamu mafuta haya bado hayajasafishwa lakini wenzetu vilevile wanahitaji mafuta ambayo yamesafishwa kwahiyo wameona fursa ya kuendelea kuitumia bandari yetu ya Tanga kupokea mafuta ambayo hayajasafishwa kutoka nje yapitie Tanga ili yaweze kupelekwa Uganda, “alisema Kitandula.
Alisema viongozi hao wamekuja kujionea miundombinu iliyopo jijini Tanga ya kampuni ya GBP ambapo wameridhishwa sana na uwekezaji walioufanya.
“Kama mlivyosikia wenyewe wamewakaribisha GBP waweze kwende kuwekeza Nchini Uganda na tayari GBP wanafanya biashara na Uganda ya kusafirisha mafuta yao nadhani hii ni fursa sasa nzuri sana ya kuendelea kuimarisha uwekezaji kati ya pande zote mbili hivyo nichukue fursa hii kuipongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika Nchi yetu mazingira ambayo yanavutia sekta binafsi kuweza kuwekeza na kufanya biashara hali inayoongeza uchumi wa nchi, faida kwa watanzania kupata ajira na wenzetu wa Uganda nao kuweza kupata mafuta ambayo ni ya bei ya chini, “alisisitiza Kitandula.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amemshuru Rais kwa kubwa anayoendelea kuifanya na kueleza kuwa serikali ya Rais Samia imeendelea kuweka nguvu kubwa katika mradi wa bomba la mafuta kutoka Nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Mgandilwa amesema kuwa wamejionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya GBP na kueleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza uchumi wa Tanga na Taifa kwa ujumla.
Mwisho.
Habari picha ni Viongozi mbalimbali kutoka nchini Uganda na Tanzania walipofanya ziara ya kutembelea kampuni ya mafuta ya GBP iliyopo jijini Tanga huku wakionyesha kufurahishwa na uwekezaji huo. Picha na Hadija Bagasha Tanga.
More Stories
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania