Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Kanisa la Moravian jimbo la Mashariki wameandaa tamasha liitwalo Rejoice Tanzania litakalofanyika Septemba 16, 2022 lengo ni kumsifu mungu na kuabudu, kuliombea amani Taifa la Tanzania na kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Moravian Efatha Choir Jimbo la Mashariki Ushirika wa Uhuru, Jacob Mwashiozya alisema tamasha hilo litakua siku ya Ijumaa katika uwanja wa Uhuru na litaanza usiku na kuisha asubuhi;
“Katika tamasha hilo tutatangaza injili ndani na nje ya nchi lakini pia pesa zitakazopatikana katika tamasha hilo litaenda kuisaidia jamii”
Aidha Mwashiozya alisema katika tamasha hilo kutakuwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Congo, South Afrika n.k, ambao ni waimbaji wa Choir mbalimbali na binafsi.
Mwashiozya alisema Maandalizi ya Tamasha hilo yamefikia asilimia 80 na Kuhusu Tiketi, alisema zitapatikana kwa shilingi 15,000 , 20,000 , 50,000 , 500,000 na 1, 000, 000
Pia Tisheti zitapatikana kwa shilingi 15,000 , 20,000 na 25,000.
Aidha Mwashiozya alisema Tamasha hilo lilianza tangu mwaka 2019 na litakua endelevu.
Kwa upande wake Mlezi wa Moravian Efatha Choir, Yona Sonela alitoa wito kwa watu wote waweze kujumuika, kumlilia Mwenyezi Mungu na kumuombea Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan lakini pia kushuhudia Choir tulizozialika na jinsi utakavyokuwa tunaiombea nchi yetu
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8