Na Hadija Bagasha Tanga,
Jamii imetakiwa kuendelea kupinga ndoa za utotoni kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa ya watoto kuzaa chini ya umri mdogo jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa wakati wa Kilele cha utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wanaliofanya vizuri katika uandishi wa Insha ulioandaliwa na shirika la World Vison na kushirikisha wilaya 4 katika Mkoa wa Tanga.
Mgandilwa alisema kuwa umri unaoruhusiwa kisheria kubeba ujauzito ni kuanzia miaka 22 jambo ambalo ameeleza kuwa kwa Tanzania sasa kumekuwepo na changamoto kubwa ya watu kubeba ujauzito chini ya umri huo ambapo wengi wao wamekuwa wakibeba ujauzito kuanzia miaka 19 kuendelea huku wakisahau mfumo wao wa uzazi bado haujakaa vizuri.
“Niwaombe kwenye pakeji yenu mnapozungumzia masuala ya ukatili tuone namna gani tunaweza kupambana na hili kwa kutoa hamasa ili watanzania waweze kupata fursa ya kujua kuwa kuna umri husika ambao wanatakiwa kubeba ujauzito na wakawa salama, “alisistiza Mgandilwa.
Aidha alilipongeza shirika hilo la World Vision kwa kazi kubwa wanayoifanya kwenye Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla kwani kumekuwepo na taasisi nyingine nyingi zinazofanya mambo ambayo hayana tija kwa jamii hivyo alitumia nafasi hiyo kuipongeza World Vision.
“Mradi huu ambao mnafanya nyie kwangu mimi ninaona ni moja ya miradi bora na mizuri kwakuwa mnatengeneza kizazi ambacho kesho kitajua umuhimu wa mambo makubwa mawili jambo la kwanza likiwa ni umuhimu wa elimu kutoa zawadi hizi kwa hawa washiriki ni kutoa hamasa kwa vijana wengine waweze kuboresha na kuona kuna sababu ya kuendelea kufuatilia sana wawapo madarasani Lakini jambo la pili ni kuendelea kupinga masuala ya ukatili unaoendelea kutendeka, “alisisitiza Mgandilwa.
“Tuna kila sababu ya kuendelea kupanua wigo wa mradi wetu leo tumeshindanisha Halmashauri 4 lakini mkoa wetu una Halmashauri takribani 11 tuna kila sababu ya kufanya ushindanishi wa hiziz Halamashairi zote ili kuwaongezea uwezo kutokana na ushandani umaokuwepo unaotokana na wigo wa watoto hawa, “alisisitiza DC Mgandilwa.
Amesema ingekuwa vyema mashindano hayo yakapewa ukubwa kutokana na ukubwa wa shirika la World vision ikiwezekana mshindi wa kwanza wamfadhili katika masomo yake ili kuendelea kukuza vipaji vya watoto.
“Pamoja na hilo ninaomba nisistize jambo lingine pamoja na kwamba tumeibua hivi vipaji ukiachilia mbali zoezi la kuendelea kuwasimamia katika miendendo yao ya kila siku tuna kila sababu ya mradi wetu ukahama kidogo wakati mkiendelea na mambo ya ukatili wa kijinsia lakini si vibaya tukatengeneza miradi mingine ya vitu ambavyo tutawakumbukeni, “alisema Mgandilwa.
Alisema yapo madawati ya jinsia katika Halmashauri na wilaya huku mazingira yao katika ofisi zao yakiwa sio rafiki kwao ikiwemo uchakavu wa miundombini ya majengo hivyo amewaomba kuwajengea ofisi za madawati ya jinsia ili kila anayekwenda kutoa taarifa ajisikie huru.
“Niwaombe tunatamani tuendelee kuwakumbuka leo, kesho na kesho kutwa ninawaomba tusogee sogee kidogo kufanya miradi ambayo kwakweli tutaendelea kuwaenzi siku zote shirika hili la World Vision, “alibainisha Mgandilwa.
Kwa upande wake Esta Mongi ambaye ni Meneja wa World Vision Kanda ya mashariki amewataka wanafunzi walioshinda katika uandishi wa Insha wakawe mabalozi wazuri katika kuelimisha jamii ikiwemo kupinga ndoa za utotoni kwa mabinti wadogo.
Alisema kuwa kwa Mkoa wa Tanga wao kama World Vision wameshirikiana wameshirikiana na baadhi ya Halmashauri Mkoani humo katika kuunda mabaraza ya watoto na kina mama huku akiahidi kuendelea kushirikiana nao kwa kuyajengea uwezo na kuwa imara zaidi ili changamoto zote za ukatili kwa watoto na kina mama ziweze kutatuliwa katika kamati hizo.
“Tutaendelea kushirikiana na nyie katika kuunda mabaraza ya watoto naamini katika miradi yetu mabaraza mengine yameshaundwa na katika maeneo ambayo hayajaundwa tutashirikiana na ofisi yako kuunda mabaraza hayo kuelimisha lengo ni ili mtoto aweze kujisimamia, kujilinda na kutoa sauti yake pale ambapo anaona kuna ukatili kwake binafsi na hata kwa mtoto mwingine, “alisisitiza Mongi.
Aidha akizungumza na kituo hiki mshindi wa kwanza katika uandishi wa Insha mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya msingi Mseko Sara Juma Mussa amesema amefurahi sana kuibuka mshindi wa kwanza na kuishauri serikali kuendelea kupambana na watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wote walioshiriki katika uandishi wa Insha katika ngazi ya Kata wamepatiwa vyeti vya ushiriki kwa unadishi wa Insha kitakachomsaidia kama kumbukumbu yake.
Kitaifa shule 544 zimeshiriki kwenye mashindano hayo ya uandishi wa Insha Kimkoa shule 42 zimeshiriki ambapo mshindi wa Kwanza kimkoa amepata laki 5 na baiskeli, mshindi wa pili kimkoa laki 4 na baiskeli, mshindi wa 3 laki 3 na baiskeli huku mshindi wa Kwanza kimkoa Sara Juma mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Mseko iliyopo wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
More Stories
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo