November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Ubongo awataka viongozi wa Dini kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa

Na David John, TimesMajira Online

MKUU wa wilaya ya Ubungo Kheri James amewataka viongozi wa Dini nchini kutumia nafasi zao kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa kwani kufanya hivyo kunatoa fursa kwa serikali kuwafikiwa wananchi wake kimaendeleo.

Amesema mwaka huu Agosti 23 ni mwaka wa sensa hivyo nivema viongozi wakahamasisha wananchi wao na kuwakumbusha umuhimun wa kuhesabiwa na ukizingatia zoezi hilo linafanyika kila baada ya miaka kumi.

James Ametoa kauli hiyo leo juni 11 mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa umoja wa Chama cha wababa (UBAKI)wa Kanisa la Angalikana Archidikonary ya Ubungo uliofanyika katika la mtakatifu barthromayo wilayani humo.

“Kwanza nawapongeza kwa uzinduzi huu wa Chama cha wababa kwani kimekuja wakati sahihi ukizingatia mara zote tumekuwa na mambo ya akina mamam tu hivyo Chama hiki ni sehemu ya juu kwa wababa katika kuwasilisha na kutoa maonin yao.lakini pia tutumia umoja huu kukumbushana juu ya kulinda maadili yetu na malezi kwa vijana wetu.”amesema

Nakuongeza kuwa “Serikali hususani Wilaya yangu ya Ubungo tunamashirikiano mazuri na Kanisa la Angalikana kupitia viongozi wake ni matumaini yangu hata katika hili la UBAKI tutaendelea kushirikiana pasipo shaka.

Pia amewahamisha waumini hao kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo hususani mikopo ambayo inatolewa bila riba kupitia halmashauri ya Ubungo,nakwamba wilaya hiyo ndio lango kuu la kuingilia mjini kati na hata stendi ya Magufuli ipo ubungo hivyo ni muhimu kuwa na dicho la kutazama fursa zilizopo za kiuchumi.

“Ndungu zangu kupitia Umoja huu tuimarisha malezi kwa vijana ,maadili ,na tuendelee kukemea wizi,ufisadi,dhuluma,ukatili na uhujumu kwani haya yote ni roho zisizokubarika katika jamii yetu”amesisitiza James

Nisisitize kuwa kuwapongeza kwa kuazisha Chama hiki cha wa Baba na shukrani kwa kanisa kuendelea kwa kazi kubwa ya kuendelea kubadilisha fikra na mitazamo.”amesema

kwaupande wake Kasisi kiongozi wa kanisa la Angalikana Dayosisi ya Dar es Salaam Richard Kamenya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha UBAKI Moses Manyata wamesema pamoja na mambo mengine yote lakinin pia watatumia umoja huo kuhamsisha waumini kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa linalotarajia kufanyika kitaifa Agosti 23 mwaka huu.

Pia wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwenye taasisi za dini hivyo wao kama viongozi jukumu lao kubwa ni kuendelea kusimamia utulivu uliopo.

katika uzinduzi huo wa Chama cha Umoja wa Baba UBAKI mkuu wa Wilaya hiyo ya Ubungo Kheri James amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya kutunisha ufuko wa umoja huo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James (kulia) akikabidhi makusanyo kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Umoja wa Wababa (UBAKI) Moses Manyatta yaliyokusanywa kutoka kwa washarika na waumini wa kanisa hilo (hawamo pichani wakati wa sherehe za kuzindua rasmi Umoja huo zilizofanyika leo Juni 11,2022 katika kanisa la Mtakatifu Batolomayo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake katika hafla hiyo muda mfupi baada ya kuzindua rasimi Umoja wa chama cha Wababa (UBAKI) wa Kanisa Anglicana katika Wilaya ya Ubungo.
Mwnyekiti wa UBAKI Mosses Manyatta akizungumza akelezea majukumu ya Chama hiyo mapema mara baada ya kuwasili mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali, wahumini na washarika wa kanisa hilo wakifuatilia hotuba za viongozi zilizokuwa zikitolewa kwenye hafla hiyo.
Viongozi wa UBAKI wakitambulishwa rasmi na kuwekwa wakfu kukiongoza Chama hicho katika hafla hiyo.