November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAKUKURU Mkoa wa Kagera yafanya tafiti utekelezaji wa miradi 28 ya maendeleo

Na Ashura Jumapili, TimesMajira Online, Bukoba

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa( TAKUKURU ) Mkoani Kagera imefanya tafiti nane katika maeneo mbalimbali na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ( 28 ) yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.4Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph, wakati akiongea na waandishi wa habari Mkoani humo.

Joseph, alisema miradi iliyofuatilia ni ukarabati wa miradi ya maji,ujenzi wa hospital,vituo vya Afya, Zahanati pamoja na ujenzi wa madarasa chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa mapambano dhidi ya Uvico 19.

Alisema tafiti hizo na ufuatiliaji ulilenga kuthibitisha thamani ya fedha ( Value for money) katika utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na kubaini mianya ya rushwa.Alisema walibaini mapungufu kwa baadhi ya miradi ikiwemo kutumia vifa vyenye ubora tofauti na ilivyoelekezwa na BOQ kutokana na usimamizi hafifu wa kihandisi,viti kutengeneza pungufu na ilivyokadiriwa kwa maelezo kuwa fedha hazikutosha,kutoweka kumbukumbu za utoaji wa vifaa kutoka stop na ukiukwaji wa Sheria na kanuni za manunuzi.

Alisema pia walibaini urushwaji wa Bei kwa baadhi ya vifaa vya umeme na ujenzi kuuzwa kwa bei kubwa kuliko bei ya soko ambavyo ni Mirunda na mbao.

“Baada ya ufuatiliaji huu imetolewa elimu kwa wahusika wa miradi Saba ili kuboresha kasoro zilizojitokeza na tayari maboresho yanafanyika na miradi Tisa uchunguzi wa kina unaendelea kufanyika na miradi ( 12 ) Kati ya 28 haikuwa na kasoro inaendelea kukamilishwa.Alisema jumla ya malalamiko ( 164 ) Kati ya malalamiko hayo ( 89 )hayahusiani na rushwa walalamikaji walielimishwa na kupewa ushauri.”

Aliongeza kuwa malalamiko 75 yalihusu rushwa na kufunguliwa majalada ya uchunguzi majalada 36 umekamilika na hatua mbalimbali za kusheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa na majadala 39 uchunguzi wake bado unaendelea.

Alisema idara zinazolalamikiwa kutokana na taarifa ( 164 ) halmashauri ni ( 108 ),Idara ya fedha ( 45 ),Idara ya elimu (10 ), maendeleo ya jamii ( 09 ),ugavi ( 16 ) maji ( 06 ),Idara ya Afya ( 19 )na watendaji wa Vijiji( 03 ).

Alisema taasisi zingine 56 zilihusu watu binafsi ( 10 ) taasisi za kifedha (05),mashirika binafsi ( NGO )4,Polisi ( 13)uhamiaji (07),mahakama ( 06 ) tanesco ( 06 ) na Chama kikuu Cha ushirika KDCU Karagwe ( 05 ).

Alisema mapya ( 6 ) yalifunguliwa mahakamani na kufanya na kufanya jumla ya mashauri (51 ) yanayoendelea kusikilizwa Mkoani Kagera. Mwisho.