Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amewataka viongozi wa vyama vya Ushirika Nchini kuhakikisha ushirika unakuwa fursa ya kuleta maendeleo nchini badala ya kulifanya ni eneo la kuzalisha migogoro.
Akifungua Kongamano la pili la Tafiti za Ushirika lililofanyika jijini hapa,Mavunde amesema,Ushirika ni eneo ambalo likitumika vyema linaweza kuisaidia nchi hata kutatua changamoto iliyopo nchini ya uhaba wa mafuta ya kula.
Mavunde amesema,sheria ya ushirika inatoa fursa kukabili changamoto nyingi hapa nchini ikwemo katika kuzalisha mafuta ya kula.
Kwa mujibu wa Mvunde Serikali inatumia shilingi bilioni 474 kuagiza mafuta nje ya nchi huku akisema,lazima ushirika uwe sehemu ya utatuzi wa changamoto hii .
“Katika makongamano haya lazima muungalie ushirika katika picha tofauti ,maana huko zipo fursa za uwekezaji ,hakuna sababu ya kuzalisha migogoro kwenye ushirika ,tunataka ushirika uzalishe utajiri,
“Haipendezi kila siku kusikia kwenye ushirika ,hali hiyo lazima ikome..,kwenye ushirika kunanyooshewa vidole kwa uovu ,lazima tuutoe ushirika huko .”amesema Mavunde
Amewataka viongozi wa vyama hivyo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,uwajibikaji na uadilifu ili kuleta tija katika tasnia ya ushirika nchini.
Aidha Mavunde amewataka wajumbe wa kongamano hilo kujadili kwa kina kuona namna kongamano hilo litatoka na utatuzi wa changamoto ya mafuta ya kula iliyopo nchini,ngano na sukari ili ifike wakati bidhaa hizo zote zipatikane hapa nchini.
Awali Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na mtendaji Mkuu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini (TCDC) Dkt.Benson Ndiege amesema,kongamano hilo ni muhimu katika kuibua changamoto za ushirika na kuzitafutia ufumbuzi.
“Tunachotakiwa hapa ni kuibua changamoto na kuziweka kwenye utekelezaji wa mwaka unaokuja .”amesema na kuongeza kuwa
“Kwa hiyo viongozi tunatakiwa kuendesha ushirika kwa mujibu wa sheria ya Ushirika.”
Akitoa maelezo ya kongamano hilo,Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Dkt.Edmund Zakayo amesema,wameamua kufanya makongamano ya tafiti za ushirika kutokana na tafiti nyingi kutokuwa na tija kutokana na tafiti nyingi kuandikwa kwa lugha ya kingereza.
Amesema,hali hiyo imefanya tafiti hizo kubaki kwenye makaratasi kutokana na lugha inayotumika katika kuyaandaa .
“Kutokana na hali hiyo ikaonekana umuhimu wa kuandaa kongamano la kwanza la tafiti za ushirika na hatimaye kuazimia kuwa na kongamano kila mwaka ili tuweze kupata fursa ya kujadiliana matokeo ya tafiti na kujadiliana changamoto zilizopo.”amesema Dkt.Zakayo
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti