April 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Brand na Partnerships (kushoto) Abella Mutalemwa akitoa zawadi kwa Abdul Msuri - Media Manager kutoka kampuni ya Dentsu kwa kusongoza kampeni iliyopata mafanikio zaidi.

Mdundo.com yarekodi idadi ya watumiaji milioni 31 katika robo ya kwanza ya mwaka 2022

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online

KAMPUNI ya Mdundo.com imetangazwa kurekodi idadi mpya ya watumiaji hai milioni 31 ndani ya Afrika katika robo ya Mwaka wa 2022 ikiwa inawakilisha asilimia 49 ya ongezeko kutoka mwaka uliopita.

Ongezeko la watumiaji wa huduma hiyo inadhihirisha ukuaji wa huduma hii katika bara zima la Afrika ndani ya mwaka uliopita.

Akizungumza jana Mkuu Brand na Partnerships kutoka Kampuni ya Mdundo,Rachel Karanu,amesema kampuni inatambua ukuaji huu kutokana na ongezeko la uhitaji wa matumizi rahisi wa huduma za muziki wa kimtandao katika jamii ya vijana pamoja na mkakati maradufu wa Mdundo na washirika ambao makampuni makubwa ya mtandao wa simu katika bara la Afrika.

Amesema katika robo ya mwaka huu kampuni pia imeongeza matangazo na washirika wake tofauti tofauti hili limechochea ukuaji huu na kuipa mdundo alama chanya zaidi.

“Tunaendelea kushuhudia ongezeko kubwa la uhitaji rahisi wa huduma ya muziki haswa kutoka kwa vijana ambao ndio wanatengeneza soko kubwa la wasikilizaji wa muziki ndani ya Afrika hii ni hitaji ambalo limepelekea ukuaji huu,”amesema na kuongeza

” Tutaendelea kujiimarisha kiteknolojia, katika uvumbuzi na njia mpya za kuongea na kuwashirikisha wasikilizaji wetu.” Amesema

Amesema mkakati wao ni kushirikisha makampuni makubwa ya mawasiliano Afrika kama MTN, Vodacom na Airtel,kwa lengo la kuwafikia wateja wao walengwa huku wakiwapatia huduma maalum iliyotengenezwa kwa ajili yao.

Aidha amesema nchi ya Nigeria na Afrika Kusini inaongoza kwa kuandikisha wasikilizaji zaidi katika kila robo ya Mwaka, ambapo Nigeria imerekodi wasikilizaji Milion 8.3 sawa na asilimia 92 na Afrika Kusini Milioni 2.2 sawa na asilimia 80.

Amesema Wasikilizaji wa Kenya wameongezeka kwa asilimia 46 kufikia watumiaji milioni 5.7 huku Tanzania ikikua kwa asilimia 10 na kufikia wasikilizaji milioni 3.8. “Kumekua pia na maongezeko ya watumiaji ya maana katika nchi za Kusini mwa Sudan, Burundi, Congo, Cameroon pamoja na Côte d’Ivoire,”amesisitiza

Karanu amesema ukiacha sababu kuu ya kutoa na kuwasilisha muziki bora na unaoongoza duniani, Mdundo pia huwapatia wasikilizaji wake Mixes za ma DJ tofauti ambazo zinaweza kupakuliwa bila kulipia.

“Tuna matajario mazuri na robo ya mwaka inayofuata huku tukiendelea katika mpango wa kufikia wasikilizaji wetu walengwa katika mwaka wetu wa fedha unaoishia Juni 2022. Tutaendeleza ukuaji wetu kupitia uvumbuzi wa kiteknolojia katika kuandikisha watumiaji wapya, pamoja na kutoa jukwaa maridhawa la matangazo kwa washirika wetu”Amesema Karanu.